April 11, 2021


BAADA ya CEO wa Simba Barbara Gonzalez kuweka wazi mipango yao ya kutumia basi lao jipya, uongozi wa Yanga nao umejibu mapigo kwa kuweka hadharani kuwa nao watashusha basi jipya na kali zaidi ya lile la Simba.

Simba na Yanga zote zinamiliki magari aina ya Yutong ambayo walinunuliwa na moja ya kampuni iliyokuwa ikiwadhamini klabu hizo mwaka 2012 ambayo wameyatumia kwa zaidi ya miaka 8.

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema kuwa ni kweli klabu hiyo ipo katika mpango wa kununua basi jipya, na la kisasa ambalo litakuwa bora zaidi ya lile la Simba ambalo limekuwa likienea mitandaoni.

“Yanga tupo katika mpango wa kushusha basi jipya kali kuliko lile TATA la wenzetu, sio kwamba mpango huu ni baada ya kuona wenzetu wameanza mchakato huo, hapana huu ni mpango wetu wa muda mrefu ambao tumekuwa nao.

“Hivyo wapenzi wa Yanga wanatakiwa kutulia kwani tutashusha basi jipya na kali kwa ajili ya kikosi chetu wanapokuwa katika safari zao za hapa na pale,” amesema kiongozi huyo.


 

8 COMMENTS:

  1. Tusimuige tembo kumeza boga

    ReplyDelete
  2. Hakuna kipindi Yanga imepata viongozi wapenda porojo Kama hivi sasa, Kama mpango wa bis jipya kali kuliko la Simba upo Kuna haja gani ya kutangaza badala ya kusubiri muda uongee? Hii yoote ni kutaka kuwaaminisha mashabiki kwamba mpo serious kumbe ovyo kabisa!

    ReplyDelete
  3. Basi la nini?kwani wanaenda mbali?

    ReplyDelete
  4. Viongozi wa Yanga mnazinguwa mjuwe badala mtafakari kuhusu timu mwenendo wake ukoje mnaanza kufanya mchakato wa kuagiza Bus jipya hivi mnaakili ninyi kama hamuwezi uongozi bhas mfanye hima msepe zenu waje watakao fanya kazi kwa moyo 1 na sio mioyo mingi kama yenu.

    ReplyDelete
  5. Wanafocus kwenye Basi wanaaahau ligi, hakika hii ndo utopolo original

    ReplyDelete
  6. Yanga wapigaji bado wengi

    ReplyDelete
  7. Mnaumiza mioyo ya mashabiki na kujitambia fahari ambazo hamzistahili kwa matokea yasiofurahisha,nadhani viongozi mnastahili fimbo nne asubuhi na nne jioni kila siku mpaka ufahamu bora uwarejee wapuuzi wakubwa ninyi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic