January 1, 2021


 MEFAHAMIKA kuwa, Yanga imemalizana kwa siri na kiungo mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama huku ikimfanyia kufuru kubwa nyota huyo.

Mzambia huyo ambaye ni kipenzi cha Simba, kama kila kitu kitaenda sawa, basi atatua kuichezea Yanga kuanzia msimu ujao ikiwa ni baada ya mkataba wake wa miaka miwili ndani ya Simba kumalizika.

 

Kiungo huyo alikuwa kwenye mipango ya muda mrefu ya kusajiliwa na Yanga ikiwemo katika usajili mkubwa msimu huu, lakini mkataba wake ndiyo ulizuia mipango hiyo kukamilika.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Kampuni ya GSM ambao ndiyo wanaofanikisha usajili Yanga, wamefanya kufuru kubwa Chama ya kumjenga nyumba ya kisasa na kifahari nyumbani kwao Zambia.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, GSM imemjengea nyumba kiungo huyo katika sehemu ya masharti aliyowapa matajiri hao huku akiomba dau kubwa la usajili ambalo huenda likaweka rekodi.


Aliongeza kuwa, pia kiungo huyo ameahidiwa gari la kutembelea la kifahari atakalolitumia katika matembezi yake ya binafsi sambamba na nyumba atakayoishi hapa nchini akiwa anaichezea Yanga.


 

"Hadi kufikia Januari 6, 2021, mkataba wa Chama na Simba unabaki miezi sita rasmi, hivyo anakuwa katika sehemu nzuri ya kufanya mazungumzo ya awali na klabu nyingine itakayomuhitaji.


“Kwani kanuni za usajili za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), mchezaji anakuwa huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayomuhitaji mkataba wake utakapobaki miezi sita.


"Hivyo, tarehe hiyo Yanga watakuwa katika nafasi nzuri ya wao kumpa mkataba wa awali, licha ya kuwepo taarifa za nyota huyo kusaini mkataba wa awali kwa siri ili Simba ambao wamiliki wa mchezaji huyo wasijue.

 

"Kwani tayari kiungo ameshajengewa mjengo mkubwa nyumbani kwao Zambia na mabosi hao wa Yanga katika kutimiza masharti ambayo Chama amewapa kama kweli wanaihitaji saini yake,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alitoa kauli ya kutisha kwa kutamka kuwa: “Tupo tayari kumsajili mchezaji yeyote kwa gharama yoyote ndani ya Afrika, kikubwa tu kocha amuhitaji.”

 

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, bilionea Mohammed Dewji, alitoa ahadi ya kumbakisha Chama Simba kwa kumuongezea mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo.

20 COMMENTS:

  1. Waandishi wasenge kama ninyi mko wengi. Hiyo hela ya gsm uliyokula ili ueneze propaganda za kuivuruga simba itakutokea puani. Endelea kuhangaika msenge wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tutumie lugha za staha tunapowasilisha maoni yetu na kuepuka mihemko hata kama habari iliyoandikwa haikufurahishi na inakukera tuvumiliane

      Delete
    2. Japo mwandishi anakera wanaturudisha nyuma wanapenda kushindana tu kila mara wavumiliwe.......

      Delete
  2. Halafu wanayanga watawadharau sana waandishi kama hawa pale ambapo watakapomwona Chama akiendelea kuwepo sana Simba

    ReplyDelete
  3. Hizi propaganda zimeanzia kwenye gazeti la Spoti Xtra la tarehe 31.12 mkaona hazijasomwa vya kutosha sasa mmezileta huku

    ReplyDelete
  4. Sasa kama kisheria mchezaji atakuwa huru kufanya mazungumzo kuanzia tr. 6 January, haya yote yanafanyikaje sasa? Au mnataka kuivuruga Simba kwa kuwa hiyo tarehe kuna mechi itakayoamua kuwa Simba inakwenda makundi au la? Tatizo hamjaijua Simba kwenye mechi ambazo wazungu wanasema " Must win Games". Subirini kuwasindikiza. Wakati wanaenda shirikisho nyie mtarudi kuwavaa Coastal Union.

    ReplyDelete
  5. Mkataba wa Chama utabaki miezi sita tarehe 21.01 2021 na si tarehe 6.1.2021. Hii tarehe waandishi wameiandika ikilenga tarehe ya mechi ya simba dhidi ya platinum fc ili kuvuruga mashabiki.

    ReplyDelete
  6. Inaonesha wazi kuwa baadhi ya waandishi wanalipwa kwa kusema uongo bila ya kujali kuwa heba ya magazeti hayo itaanguka lakini hawajali kwakuwa pesa ni mbele

    ReplyDelete
  7. Haya mahabari yenu yametukera habari zenu zinatia kichefuchefu kula sku chama

    ReplyDelete
  8. Si huyo salehe na blog yake hawana cha kuandika mbona hawachambuwi droo ya jana

    ReplyDelete
  9. Nguruwe fc mbona mbona mipovu kama yote kwa CHAMA kuondoka? Yule hana ni mchezaji na mpira ndo ajira yake . Sasa unapoona tetesi za CHAMA kuondoka ukajifanya kujua sana kutukana nadhan ni upungufu wa akili na umasikin wa fikra.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Busara kubwa ni kauli na lugha sioni sababu ya kuwaita wenzio kwa aina hiyoo ya mnyama

      Delete
  10. Mbona hamsemi kinachoendelea kwa calinhos wenu mmeng'ang'ania ya wenzenu, tumeshawajua lengo lenu. Wenye upungufu wa akili na umasikini wa fikra ni hao wanaondesha propoganda za kijinga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi niulize
      Kuandika habari ambayo haina uthibitisho je kitaaluma ya habari ikoje?!

      Delete
  11. hivi mwandishi ana akiri kweli!! Anazungumza nini hapa? Hiyo nyumba kaiona??

    ReplyDelete
  12. Nyumba ya Chama ameijenga mwenyewe kwa pesa zake anazopata kutokana na "mpira" wake. Chama alikiri mwenyewe kuwa Simba imemfanya apate vitu ambavyo hakuwahi kuwa navyo tangu aanze kucheza mpira (ref. Mwanaspoti)

    ReplyDelete
  13. Uyu mwandishi nahic analiwa na Gsm sio bure hajui mkataba wa chama unaisha lini wala tareh y kubakia miez 6 hajui anabuni t et tar 6 kwakua simba anacheza iyo ter unadhan utawatoa mchezoni kua Makin utahazwa mimba na hao mabasha wako ukajifungua sura y ingnia

    ReplyDelete
  14. Jaman si kila lizngmzwalo yanga wanahusika waandishi wengne wanaandka kwa matakwa yao tu

    ReplyDelete
  15. Soka bongo nendataratibu nishuke

    ReplyDelete
  16. Mwandishi mpumbavu sana huyu anaropoka tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic