May 5, 2021


OFISA Habari wa Klabu ya soka ya Simba SC, Haji Manara amesema kwasasa ubora wa wachezaji wa Simba ni mkubwa sana ukilinganisha na wachezaji wa Yang na amedai kama kungekuwa na usawa Yanga ingeshuka daraja.

 

Manara ameyasema hayo leo kupitia East Africa Radio alipokuwa akiongea kuhusu kuelekea kwenye mchezo wa watani wa jadi Jumamosi Mei 8, 2021.

 

”Ukitazama wachezaji wa Yanga SC kama kungekuwa na fair wangeshuka daraja, kwasasa wapo nafasi ya pili ni kwasababu ya ukubwa ukubwa tu lakini hawana ubora wa kuifikia Simba SC, iko mbali sana,” amesema Manara.

 

Aidha Manara ameongeza kuwa wamejipanga kuwafunga Yanga na kuchukua ubingwa kabla ya mechi 5 ligi kumalizika kisha wakapambanie ubingwa wa Afrika kwenye klabu bingwa.

 

”Kwanza tunaanza kumfunga Yanga SC kisha tunachukua ubingwa kabla ya mechi 5 za ligi kumalizika kisha tunaenda kushughulikia kombe kubwa Afrika. Hakuna mjadala huu ubingwa wa Tanzania tunachukua miaka 10 mfululizo,” ameeleza.

 

Mchezo huo utarushwa moja kwa moja na Global Radio kuanzia saa 10:00 jioni ambapo utafanyika uchambuzi kabla ya mechi, matangazo ya dakika 45 za kwanza, uchambuzi wakati wa mapumziko, dakika 45 za mwisho na uchambuzi baada ya mechi.

6 COMMENTS:

  1. Simba wakienda kimzahamzaha mbele ya Yanga basi wataangukia pua.Wanatakiwa kutoamini uwezo wao wa mpira peke yake kuwa ndio njia pekee ya kuishinda Yanga. Ili kuishinda Yanga kiulaini simba wanatakiwa kutumia mbinu zaidi hasa za ndani ya uwanja. Hakuna asiejua kuwa mabeki wa Yanga kiukweli wanabebwa na marefa ila ni mabeki wenye kucheza rafu nyingi za hovyo.Hivyo Morrison ni Mpango mzima kwa simba. Wakimsomesha vizuri jinsi ya kucheza na mabeki wa Yanga basi Yanga hawawezi kumaliza mechi wakiwa kamili.

    ReplyDelete
  2. Safari hii hatukubali mambo ya kihuni yatawale uwanjani, watu wacheze mpira na refa awe makini. Kama kuna vibahasha chukueni lalini muwe fair ila msubiri kudaiwa na waliowapa huo mlungula

    ReplyDelete
  3. Morrison awasumbue ndni ya 18 ili zipatikane penati na kadi nyekundu za kutosha. Hii ndio njia pekee ya kumkomoa beki anayetegemea rafu kuliko kukaba

    ReplyDelete
  4. Acha kuota penalty,sana sana atadaka mipira..hehe

    ReplyDelete
  5. Ndoto za mchana, derby ngapi zimepita wacheaji wanaonekana bora kama Chama na Kondeboy wanachemka, derby haina mwenyewe, sanasana Saido anaweza kuwatundika kwa uzoefu wake,kama alivyo wapiga taifa starts

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic