MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa kinachoikwamisha Yanga ni namna ya kutafuta wachezaji, jambo ambalo limekuwa likiifanya timu hiyo kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.
Pia ameongeza kuwa huenda kuna makundi ndani ya Yanga jambo ambalo haliwekwi wazi jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi.
Mwalimu amesema :-"Moja ni kwamba sijui ambaye anafanya scout ni nani, leo ukiingia Yanga ukiuliza nani aliwaleta hawa, watu watatafutana pale kwa sababu mambo sio mazuri wanajua kutuaminisha sana kwamba timu ni nzuri ila mwisho pale mambo yanapoharibika hakuna anayeweza kutoa maelezo nani alimleta huyu.
"Kwa mfano msimu uliopita alikuja mchezaji mmoja hivi ambaye ni Yikpe, (Gnamien) ambaye kwa kumuangilia sio kariba wa Yanga ni aina ya Veteran fulani hivi.
"Tulipojaribu kufuatilia quality (ubora) ya Yikpe watu walikuwa wanacomplain, (lalamika) na nilijua kwamba hatakaa, alikuja Molinga, (David) kwa shangwe nyingi na mwisho wa siku hakudumu.
"Ukiwatazama wachezaji waliopo kwa sasa ni nani ambaye anaoparate,(simamia) ukija kumtazam Saido Ntibanzokiza, huyu naye umri umekwenda kidogo na majeraha, Carlinhos, (Carlos) simuoni kama mchezaji anayeweza kucheza Physical footbal kitu ambacho hakiwezekani kwa ligi ya Tanzania ni ngumu, Yacouba anaumwa, Michael Sarpng huyu naye anakimbiakimbia tu, mechi zaidi ya 21 mabao manne.
"Hivyo cha kuanza hapo ni kujua nani ambaye anawaleta hawa wachezaji kisha mwalimu akahukumiwa lakini wakishakuja nini kinatokea ndani ya Klabu ya Yanga, inawezekana kuna makundi, ila tunachojua ni kwamba mwalimu huyu amekuja kisha akaondoka," alisema Kashasha.
Kwani Yanga imeshuka daraja?mpaka ionekane imekwama .
ReplyDeleteUsimsikilize kashasha... Sisi yanga tunampenda sarpong kwa mikimbio yake tu
DeleteUpo sahihi
DeleteMZEE KASHASHA UPO SAHIHI YANGA WANAFELI KWENYE USAJILI, WANASAJILI WACHEZAJI WABOVU WALIO SHUKA VIWANGO KUTOKA NJE NA KUWADANGANYA WANACHAMA NA MASHABIKI WAO KUWA WAMESAJILI VIFAA KUMBE NI MAGARASA, HIZO NI MBINU ZA KUUZA JEZI TU. GSM WANALENGA KUPATA FAIDA KWA MAUZO YA JEZI HAIJALISHI WANAMSAJILI NANI.
ReplyDeleteWewe muandishi hunipendi Yanga hata kidogo nakujua hushawai kuandika oungo Yanga dhidi ya Cost ulipost 2-0 wakati vilikuwa 1-0
ReplyDeleteMwandishi uchwala