WEKA kando hasara ya muda na nguvu ambayo ilipatikana Mei 8 baada ya mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga kughairishwa kutokana na Klabu ya Yanga kugomea mabadiliko ya mchezo huo.
Karikaoo dabi kwa msimu wa 2020/21 mabadiliko yake
yamefanywa raundi zote mbili ambapo ile ya kwanza mambo yalikwenda sawa ila hii
ya pili mambo yalibuma.
Zipo mechi nyingine ambazo zilifanyiwa mabadiliko na mechi
zilichezwa kama kawaida hizi hapa baadhi yake twende sawa:-
Yanga 0-1 Azam FC
Mchezo huu ulipangwa awali kuchezwa saa 1:00 usiku
ulipelekwa mbele mpaka saa 2:15 usiku ilikuwa ni Aprili 25. Taarifa ilitolewa
Aprili 21 na Bodi ya Ligi Tanzania ambapo ilieleza kuwa sababu kubwa za
kubadili muda wa mchezo huo ilikuwa ni Uwanja wa Mkapa kuwa na matumizi
mengine.
Simba 2-2 Azam FC
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 7, ulipaswa kuchezwa saa 1:00 usiku na badala yake muda ukarudishwa nyuma mpaka saa 10:00 jioni.
Sababu kubwa ya kufanya mabadiliko hayo ilikuwa ni changamoto ya miundombinu iliyoathiri uwakaji wa taa. Taarifa hiyo ilitolewa Februari 6 na mechi ikachezwa Februari 7.
Pia taarifa hiyo ileleza kuwa nchi mbalimbali bado ziliendelea kuweka masharti magumu katika taratibu za usafiri wa kimataifa tangu kuzuka kwa janga la virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.
Taarifa ya mabadiliko ilitolewa Oktoba 7 na mechi ilichezwa Novemba 7.
Ligi Daraja la Kwanza
Sio ndani ya Ligi Kuu Bara pekee ila mpaka Ligi Daraja la Kwanza pia mabadiliko yapo. Oktoba 25,2020 mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Majimaji dhidi ya Mawenzi Market uliopaswa kuchezwa Oktoba 25 ulipelekwa mbele mpaka Oktoba 26.
Sababu kubwa ya kufanya hivyo ilikuwa ni timu ya Mawenzi
Market kushindwa kufika kituoni kutokana na kupata ajali maeneo ya Iringa
wakati wakielekea Songea. Mchezo huu ulichezwa siku ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment