May 11, 2021


 ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba miaka ya 
nyuma, Dylan Kerr, ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kuipa ubingwa wake wa kwanza Klabu ya Tshakhuma Tsha Madzivhandila (TTM FC) inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.


Kerr ambaye alikuwa kocha wa Simba mwaka 2016, ameweka historia kwa kuipa timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 Kombe la Nedbank baada ya kuwachapa Chippa United 1-0, mchezo ukichezwa wikiendi iliyopita.

TTM ambayo ipo kwenye vita ya kujikomboa kwenye kushuka daraja, iliweka rekodi ya kutwaa kombe hilo na kuvuta kitita cha Randi milioni 7 (Sh bilioni moja na milioni 154) ikiwa imekaa kwenye ligi kwa msimu mmoja pekee.


Kerr aliwahi kupita Simba mwaka 2016, kisha akatimkia Kenya kujiunga na Klabu ya Gormahia FC, kisha Baroka FC na Black Leopards, zote za Sauz.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic