May 11, 2021

 

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu,  Didier Gomes raia wa Ufaransa leo Mei 11 kimewasili salama nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa robo fainali ya kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs. 

Safari ya Simba ilianza usiku wa kuamkia leo katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere majira ya saa 9:00 usiku.

Kilipitia Kenya kwa Shirika la ndege la Kenya Air Ways kisha kiliunganisha moja kwa moja mpaka Afrika Kusini ambapo kilipokewa na watangulizi wake waliotangulia kabla ya safari.

Patrick Rweyemamu,  meneja wa Simba amesema kuwa kila kitu kipo sawa na watapambana ili kupata matokeo mazuri. 

Mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Mei 15 nchini Afrika Kusini na ule wa pili utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamekwea pipa ni pamoja na Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Luis Miquissone na John Bocco.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic