KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis
Baraza, amefunguka kuwa ameweka mkakati
wa kuhakikisha wanapata matokeo kwenye
mechi nne zilizosalia ili wajinusuru na janga la
kushuka daraja msimu huu.
Kagera Sugar inapambana kujinasua na janga la
kushuka daraja kutokana na kuwa na
mwenendo usioridhisha kwenye Ligi Kuu Bara
baada ya kukusanya pointi 33 kwenye mechi 30
walizoshuka dimbani hadi sasa, wakiwa katika
nafasi ya 13.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Baraza
alisema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea mechi zetu za mwisho ambazo zimebakia, najua ugumu ambao upo kwenye ligi kutokana na kila timu kupambana kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutoshuka daraja.
"Kwenye mechi nne ambazo tumebakiwa nazo ni lazima tupambane kuhakikisha tunapata matokeo ili tuweze kujinusuru na janga la kushuka daraja.”
Kagera Sugar imebakiza mechi nne kumaliza Ligi
Kuu Bara msimu huu ambazo watashuka
dimbani dhidi ya Polisi Tanzania, Prisons, Ihefu
na Coastal Union.
0 COMMENTS:
Post a Comment