BAADA ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen leo kutangaza orodha ya wachezaji 27 wa timu hiyo, imeelezwa kuwa nyota Hassan Dilunga alikuwa kwenye orodha ya kimaandishi kimakosa.
Orodha ya kwanza ilijumuisha wachezaji 27 na jina ambalo liliandikwa katika wachezaji hao ni pamoja na kiungo wa Simba, Hassan Dilunga.
Taarifa ambayo imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa yalifanyika makosa katika uandishi.
"Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 27 watakaoingia kambini Juni 5,2021. Kwa bahati mbaya katika kikosi kilichotolewa kwa maandishi kimeonesha mchezaji Hassan Dilunga ameitwa ikiwa ni makosa ya kiuandishi, Dilunga hajajumuishwa kwenye kikosi kama video inavyomuonesha kocha akitaja kikosi.
"Vilevile mchezaji Mudhathir Yahya ambaye ameitwa hakuonekana kwenye kikosi cha awali, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza," ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari, Cliford Mario Ndimbo.
Upuuzi tu yani
ReplyDeleteSiasa na ujanja ujanja mwingi
ReplyDeleteYaani hata kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya Taifa TFF wanasogeza mbele majina!!!!!!
ReplyDeleteMeechapishaa mtandaoniii hayaajaakaguliwaaa mmmh tifutifuu mnaaupelekaa wapii mpira
ReplyDeleteKuna kiongoz hapo alipiga panga jina la mudathir ili aende dilunga lkn ikashkndikana mwishoni
ReplyDelete