May 28, 2021


 Na Saleh Ally

INAWEZEKANA nikawa sikufurahishi kutokana na kuwataja wachezaji vipenzi vyako na ushauri wangu ukawa ni kuona wanaachwa, sitajali. Lakini soma kidogo kwa kuwa hawa, naona wanachukua fedha za bure Yanga.


Yanga inapaswa kupata huduma kutokana na kile ambacho inakilipia kwa maana ya kutoa huduma ya mishahara mizuri na huduma nyingine kwa wachezaji wake na hasa wale wa kigeni, sasa wanafanya nini?

 Tujiulize wanaipa Yanga kinachostahili? Binafsi naona hapana lakini naiona hapana hii ingeweza kuwa na nafuu kama ungeona wachezaji hawa wana majuto, wanaonyesha kusikitishwa kulingana na kile wanachoifanyia Yanga lakini imekuwa tofauti.


Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakionyesha ujeuri

wa wazi, wamekuwa wakiamini wao ni wakubwa ikiwezekana hata kuliko Yanga yenyewe na huenda wanaamini Yanga haiwezi kwenda bila ya wao.


Kuna mambo matatu makubwa, moja kiwango duni, pili majeruhi na tatu nidhamu mbovu ambayo inaipa Yanga kila sababu ya kuachana na rundo la wachezaji wake wa kimataifa.


Ukiangalia, sote hata Yanga wenyewe hawawezi kukataa ubora wa kiwango cha watani wao, Simba.

Ukiangalia mchango mkubwa wa kiwango bora cha

Simba, bila ya ubishi unatengenezwa na wachezaji

wa kigeni. Wachezaji wa kigeni wa Yanga mchango

wao ukoje?



Mechi zikiwa zimebaki tano kufunga msimu huku Yanga wakiwa wanaufukuzia ubingwa kwa asilimia 35 na zilizobaki ni nafasi ya pili, unaona takribani nusu ya wachezaji wake wa kigeni wako nje ya uwanja wakiwa na matatizo kadhaa, mfano utovu wa nidhamu, majeruhi, kiwango duni au matatizo ya kifamilia.


Wachezaji walio nje bado hawaonyeshi kama kweli wana majeruhi, kwa hali ilivyo bila ya ubishi, baadhi yao inaonekana wamesusa katika kipindi hiki kigumu ambacho Yanga inawahitaji kupambana kwa ajili ya ubingwa na wakiukosa basi kujihakikishia nafasi hiyo ya pili.


Angalia, Azam FC sasa wanaifuata Yanga kwa mwendo wa kutisha kidogo na wamekuwa na mwenendo mzuri. Jambo ambalo Yanga inahitaji kikosi kipana ili kupambana na kuhakikisha wanamaliza katika sehemu hizo mbili za juu.


Hakuna ubishi kama Yanga watazubaa kidogo wanaweza kuingia kwenye mshituko wa kujikuta katika nafasi ya tatu. Lakini angalia wachezaji wa kigeni na wale wa kutegemewa karibu asilimia 60, wako nje ya uwanja kwa sababu ambazo nyingi ni vijisababu.

Carlinhos ni mmoja wa wachezaji wazuri lakini hata mara moja hajawahi kuichezea Yanga zaidi ya mechi tano mfululizo. Mchezaji wa on, off na kweli akicheza mchango utauona lakini anacheza mechi ngapi angalau mfululizo. 

Angalia wachezaji wa Simba, nani na yupi unaweza kumkosa kila mara kama ilivyo kwa Carlinhos. Kwa uzuri tu Yanga wamuonyeshe njia aende zake.


Sijajua mikataba yao wameipanga vipi na kama kulikuwa na tahadhari, lakini mshambuliaji Michael Sarpong naye hana faida, mabao manne hadi leo na zaidi ya hapo ni mbwembwe tu, hakuna kingine kilichofanyika. Yanga wanapaswa kumuonyesha mlango mapema sana kwa kuwa ni hasara kuendelea kubaki naye, wa nini sasa?


Hawa veteran wawili wa Kirundi, Saido Ntibazonkiza na Abdulazak Fiston nao hawana mchango ambao Yanga wanaweza kujivunia na ukweli ni kwamba wanatumia muda mwingi wakiwa nje ya uwanja.


Mchango wao ni mdogo na mbwembwe ni nyingi, sema mashabiki wa Yanga wanataka furaha, anayewapa kidogo wanaichukulia kama nafuu kubwa lakini kiuhalisia, bado Ntibazonkiza na Fiston hawajafanya kitu kikubwa ambacho Yanga wanaweza wakajivunia sana.


Umeona Fiston akiwa kwenye insta Live akichati na mashabiki wakati Yanga ikipambana uwanjani. Unaweza kusema angeweza hata kutumia muda mwingi kuangalia mchezo na kujua wenzake wanafanya nini. Ntibazonkiza mara ya mwisho kufunga ni lile bao alipoingia akiwa na hasira baada ya Kocha Juma Mwambusi kumuacha nje, akafunga na kuomba atolewe.


Lakini tangu alipoanza kupewa nafasi ya kuanza,

hajafunga. Ukweli kwa maana ya hadhi ya

wachezaji wa kulipwa wanaofanya kazi yao Yanga

vizuri, hakuna kitu na wanastahili kupigwa chini.


Lamine Moro sote tumeona, inawezekana kuna

jambo la kusuluhisha kati yake na Yanga na kama

limeshindikana, basi naye apigwe chini. Yanga

inahitaji watu watakaoipa msaada hasa kwa maana

ya kuilipa kutokana na kile inachowalipa.


Niwakumbushe, kama wageni wanalipwa zaidi basi

nao wanastahili kutenda na kufanya vizuri zaidi. La

sivyo, wakubali kufanya kazi kwa kiwango cha chini.


Mshahara wa Sarpong ukijumlisha na utovu wa

nidhamu ni hasara tu kwa Yanga na lazima uongozi

Yanga ubungue bongo kwamba kinachoendelea ni

kuendelea kujiumiza lakini anayeumia hataki kupiga

kelele kwa sauti ya juu kwa hofu ya kuona majirani

watamsikia, hivyo amebaki kugugumia tu maumivu.

7 COMMENTS:

  1. Wacha maneno kwahiyo sapong na saido na kalinyos watemwe.

    ReplyDelete
  2. Takataka za manara ndo hizi, huyu kaandika nn kama siyo ushuzi

    ReplyDelete
  3. Shida ya manazi ya Utopolo hampendi kuambiwa ukweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba mulitaka lini kuambia ukweli huyo mwenyewe anatumika na mikia hatutaki ushauri wa kimama huo sie tutapambana wenyewe nyie jisifieni na tff yenu

      Delete
  4. Maranyingi Saleh Jembe anaangalia udhaifu wa Yanga, huwezi kuona anakosoa Cimba, unaweza ukafahamu nia yake kwa Yanga sio kujenga baki ni kubomoa, kikubwa wanaYanga kufanya mambo yao kwa Uweledi wa haki ya juu, wasio watakua mema ni kikundi cha watu wachache kinacho paza sauti kuwavuruga, Lkn Daima mbele nyuma mwiko...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic