May 10, 2021


Na Saleh Ally

KUNA kanuni, kuna sheria na hizi zinapaswa kufuatwa lakini mbele yake kuna busara ambayo inapaswa kutumika juu ya hizi kwa lengo jema kabisa.


Achana na ile kauli ya sheria zimeundwa ili zivunjwe, lakini unaweza kusema busara imekuwepo ili kuokoa kila kinachoonekana kinakwenda mrama na kuizidi nguvu sheria au kanuni ambazo zinakuwa zinaongoza jambo fulani.


Sheria zinaundwa na wanadamu, lengo ni kukiongoza kitu kwa kusimamia utaratibu ulio sahihi na kunakuwa na wale ambao wamekabidhiwa kuusimamia utaratibu huo, kuna wakati hata wao hukosea.


Uongozi wa Yanga, juzi umepitisha uamuzi wa kuitoa timu yao uwanjani wakieleza namna Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuvunja kanuni ya ubadilishwaji wa kanuni ya kubadilishwa kwa muda wa mechi

ambayo inaagiza angalau saa 24 kabla ya muda

sahihi wa mechi. Yanga wameamua kufuata kanuni, wameamua kutoa timu uwanjani baada ya kupewa taarifa mapema taarifa ya kwamba mechi itaahirishwa lakini haikuwa ndani ya saa 24.


Katika hali ya kawaida kulikuwa na mambo ya

muhimu kujifikiria kuhusiana na suala hili. Na mimi

na wewe twende tuliangalie namna hii, kwamba

kweli uongozi wa Yanga umefuata kanuni, hawana

kosa. Lakini tujiulize walijifikiria madhara ya

kutovumilia saa 2 tu zilizokuwa zimesogezwa

mbele?


Tujiulize, uongozi wa Yanga kama ungeacha timu

yake icheze baada ya saa 2 mbele, nini ambacho

ingepoteza kwa timu kusubiri saa mbili. Maana

hakukuwa na suala la kuahirisha badala yake

kusogezwa mbele (delay) kwa saa 2 tu mbele.


Saa hizo mbili halikuwa agizo la TPLB wala TFF,

lilikuwa ni agizo la Serikali ya Jamhuri ya Tanzania

kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na

Michezo. Jiulize, kuna mawasiliano yoyote viongozi

wa Yanga walifanya na wizara kutaka kujua undani

wa suala lililowalazimisha wao kuchukua uamuzi

huo?



Si vibaya tukisema wizara na Yanga ni wale

wanaofanya kazi sehemu moja, maana yake ni

rahisi kufungua mashauriano kuhusiana na jambo

fulani ambalo linakuwa limetokea kwa lengo la

kujenga au kufanya jambo fulani. Walijaribu hilo kwa kuwa tayari TPLB waliwaeleza kwamba lilikuwa ni

agizo la wizara ambayo ndiyo Serikali.


Haya yote hayakufanyika kwa kuwa uongozi wa

Yanga huenda waliliangalia suala hili kishabiki tu na

binafsi naona lilikuwa linawezekana kujadiliwa kwa

udogo, halafu kuangalia kifanyike kipi kilicho sahihi

kuhakikisha mechi inachezwa kwa kuwa Yanga

walishafanya maandalizi yao na hadi wanapeleka

timu uwanjani walikuwa tayari kwa mchezo, saa 2

mbele zingefanya maandalizi waliyokuwa nayo

yayeyuke?


Kubwa zaidi ambalo tunapaswa kumshukuru Mungu

ni kuhusiana na kwamba watu walitoka angalau

salama uwanjani na hakukuwa na maafa na hili

huenda lingekuwa la kwanza kabisa kwa viongozi

wa Yanga na wakaribu wao kulifikiria tena kwa

kiwango cha uongozi na si viongozi kuwa

mashabiki.


Narudia, saa 2 mbele zingeharibu vipi maandalizi ambayo Yanga walikuwa wamefanya kwa ajili ya mechi hiyo? Watu tayari walikuwa uwanjani na kama Yanga wanatoa timu, lingetokea suala la hasira na wao kuamua kufanya vurugu, kwa idadi ya watu zaidi ya 40,000, nani angeweza kuwazuia? Yangetokea maafa nani alipaswa kulaumiwa?



Bila shaka aliyeamuru timu kutoka uwanjani, bila ya kufanya mashauriano na mmoja wa wadau wao ambao ni TPLB na TFF ambao lazima waliwaeleza kuwa ni Serikali na wao wangewafikia!


Najiuliza, kwamba viongozi wa Yanga walishindwa kuona kunaweza kuwa na maafa na uvumilivu wa saa 2 mbele ndiyo uliwashinda, au uliharibu maandalizi yapi kwa kikosi chao na vizuri zaidi, wasingecheza peke yao. Maana hata wapinzani wao Simba pia walilazimika kusubiri hizo saa 2 kama walivyokuwa wameelezwa. 


Sasa tofauti ni nini hapo? Viongozi Yanga walifikiria usumbufu wa fedha za waliokuwa wameingia uwanjani? Au waliona haliwahusu kwa kuwa wenyeji wa mechi ni Simba?

Lakini wanajua hata mashabiki wao pia walilipa? Bado hawakujiuliza watu wametoka mbali kwenda kuiunga Yanga mkono pale Benjamin Mkapa.

Achana na yule aliyesafiri kwa miguu kutoka Kigoma, wako wale ambao waliingia uwanjani tangu saa 4 asubuhi wakaisubiri Yanga kwa zaidi ya saa 7 na yenyewe ikashindwa kusubiri saa 2 mbele!

Lazima tukubali, kuna shida kubwa hapa kwa viongozi wa Yanga na hakika walishindwakuonyesha busara na weledi wa uongozi kama wazazi na wakaamua mambo kishabiki, jambo ambalo huenda lingeweza kuleta madhara makubwa.Tumeona Polisi walilazimika kupambana na baadhi


ya mashabiki waliokuwa wakitaka kurudishiwa fedha zao, wakarusha mabomu ya machozi na hakukuwa na madhara makubwa. Hili ni jambo la kushukuru lakini kuwasisitiza viongozi Yanga, wakati mwingine vizuri kutumia ukomavu, uzoefu, weledi na busara ikawaongoza kwa nia njema kabisa kwa kuwa wakati mwingine, madhara yanaweza kuwa makubwa na mwisho tukaishia kujilaumu kwa kuamua mambo kwa mihemko.

17 COMMENTS:

  1. Kisha jiulize aliyetoka Morogoro au Mlandizi aliyetaka atazame mechi hiyo kisha saa moja jioni apate usafiri wa kurudi kwake je walitazama hilo walioahirisha? Nenda kwenye mifano hiyo kwa busara ya upande mmoja kisha igeuzie kwenye muda ambao washabiki wangeupoteza pasipo sababu za kimsingi kwanini walikatisha tiketi kisha kuruhusu watu waingie kiwanjani?

    ReplyDelete
  2. Pamoja na insha ndefu uliyoandika muhimu nikuwa uvunjifu wa sheria unapaswa siku moja kukomeshwa na hizi ndo dalili ya kutimia hili

    ReplyDelete
  3. Na unapozungumzia hili jaribu kuangalia na hali na madhara ya mashabiki waliotoka sehemu mbali mbali so busara kwao ilikua iwe nini.tupige vita ukiukwaji wa sheria bila sababu ili kuondoa ukanjanja na kupotezeana muda ni mali

    ReplyDelete
  4. Busara ni kufanya jambo kwa wakati, sio ubabaishaji, tuache mazoea kuna watu walitakiwa kusafiri baada ya mechi hao tunawsaidia vp au mnaongea tu ilikuwafariji TFF?

    ReplyDelete
  5. kweli saa mbili ziliwashinda kuvumilia.
    kama ni kanuni basi iwe kote kote..na Yanga wawe wazi inapotokea kanuni kukosewa wanabebwa...Ni kanuni ipi sawa ilimfanya mwamuzi wa mechi na TZ Prison kukataa penalti ya Prisons, ni kanuni ipi sawa ilifanya mwamuzi wa mechi Simba na Yanga kutoa penalti ya Kisinda wakati faulo imetokea nje ya 18..Wakishikilia kanuni iwe kote kote..sio ikwa muda umebadirishwa kwa Biashara sawa, Azam sawa,ikiwa Simba hatutaki
    Keto zote sababu ya kushindwa kuvumilia saa mbili.
    Kwa mziki wa Simba hata Kaizer Chief wakikimbia nduki...hatushangai

    ReplyDelete
  6. Kwa wale mashabiki waliokataka go and return ya ticket ya ndege . Je busara yako ni kusema ni wachache haitaathiri kitu hata busara yako mwandishi haina mantiki. Je serikali inaruhusiwa kuvunja sheria na kanuni kisa eti serikali imesema? Fikiri kabla ya kuandika makala ambazo hazina mashiko katika umma wa mpira wa miguu.

    ReplyDelete
  7. Umesema kweli kabisa mwandishi. Yanga kama waliona kuna 5atizo walipaswa kucheza under protest, hiyo ndio taratibu ya mpira sio kukimbia mechi. Yanga wameendeshwa na ushirikina wasijifiche kwenye kanuni ni waongo.

    ReplyDelete
  8. Good riddance.Kusema kweli inaweza kuwa ni jambo jema na lenye baraka Yanga kukataa kucheza na Simba.Wanacheza rafu nyingi sana wastani zaidi ya 15 katika mechi na kadi hawapati..Angalia mechi na Polisi upuuzi wafanye wai hslafu Yondani apate nyekundu.Pia hivyo na Prison.Mechi yao na Tanzania Prison walicheza rafu 18 na cha kushangaza yule mwamuzi aliyekataa penalti dhahiri shahiri ya Prison, alitoa kadi nne tu kwa Prison. Kuna uwezekano Ninja na wengineo angemuumiza mchezaji tegemezi strika wa Simba na labda asingekuwa fiti kucheza Afrika Kusini.Manara kasema kweli wanacheza rafu sana..tatizo ukame wa Kombe unawafanya wanatumia mbinu sizo.utopolo ni hasidi

    ReplyDelete
  9. Ndugu kwenye hili suala kwa Leo umeandika utumbo tu maana hakuna busara kama MTU mwenyewe hatendewi haki na chombo husika.Hata wizara yenyewe kupitia aliyetoa taarifa ilipaswa kutambua kuna watu wamekata tiketi za ndege ili baada ya game warudi kwako.je iwapo mchezo huo ungechezwa hao mashabiki wangerudishiwa nauli zao kwa kuwa walishakata tiketi? Jibu ni kwamba hatufanyii kazi matamko tunazingatia kanuni zinavyoeleza.

    ReplyDelete
  10. Saleh hapa kwenye hili suala umechemka kabisa. Kama ungekuwa huna cha kuandika kuhusu hili suala ni bora ungekaa kimya kabisa

    ReplyDelete
  11. Yaani mwandishi nzima unaandika utumbo kama huu? Sababu yenyewe ya kusogezwa mbele mpk sasa haijulikani sasa kuna haja gani ya kutii kitu usichokijua

    ReplyDelete
  12. Naona kelele zinakuwa nyiingi, kama simba walikuwa sahihi kucheza hio saa1 kwakuwa yanga hawakuja wamegoma nadhan sheria ziko waz, kwamba kwa muda huo simba si wangepewa point 3? leteni sababu za kusogeza game mbele, mnabwabwaja tu

    ReplyDelete
  13. Mimi labda nianze na tff maagizo kutoka wizarani sio tatizo,Bali wenyewe walihoji suala la kupeleka mbele mechi ni nn kwa wizara na pili wkt wanaitaarifu vilabu,je viliridhika?hayo ni ya kujiuliza,hitimisho,mtazamo wngu ni kwmba wahusika waliweka limit milango kufungwa saa kumi,lkn wakaona mashabiki ni wengi wasogeze mbele ili kupata hela nyingi ya mapato mlangoni,kwa kifupi watu waliangslia hela na c Moira,kama ingekuwa mpira bac ungechezwa mda husika kwn ttzo lingekuwa wapi,msipotoshe watu bhana

    ReplyDelete
  14. Mimi nadhani busara iliyofanya mechi kuhairishwa toka Feb mpaka Mei ndiyo ungezungumzia ,masaa ni mwendelezo wa upuuzi ,ungejiuliza fevour anayopewa Simba kwenye ratiba usingeandika hii makala,Jana tu sijui leo wameondoka bt mechi inachezwa Wkend wao Ratiba yao wanaamua Kama wanavyotaka,kwanini wasingecheza Ligi WK hii? Haya ma blog mnayamiliki,Lakini ungekuwa na busara ungehoji why Simba inacheza mechi kila baada ya wiki brother siyo propaganda hizi mmetuumiza muno hacha tuwakomeshe

    ReplyDelete
  15. SALEHE Ally huwezi kusifiwa kwa kujifanya mjuvi au mweledi wa makala. Ukiwa mwandishi wa habari hususani hizi za michezo zingatia sana umakini na usawa katika makala zako. Makala zako zinasomwa na Watu wengi sana ndani na nje ya nchi pia. Hapa unaweza kuandika chochote unachotaka na hakuna wa kukuzuia, ila kitaaluma utakuwa unapunguza mipaka ya wateja wako.
    Hoja zako juu ya Yanga kushindwa kuvumilia saa 2 tu umesema walikosa busara, eti sio ungwana!?
    Hivi unajua tafsiri ya Busara mkuu? Anyway huwezi kukosa kuijua mwandishi maarufu kama wewe labda unataka kusifiwa na Watu wanaofanya ujinga huu kila siku katika soka letu.
    Busara unayosema ilikosekana siku nyingikwa tff na hata baadhi ya wadau wa mchezo wa mpira. Tff wao wanaamini katika kanuni na sheria lakini imani hiyo huwa butu kwa baadhi ya timu wanazozipenda yaani timu zao. Ila kwa timu zingine huwa wanahubiri sheria na ndiyo sheria hiyo hiyo Yanga wameitumia kuwakumbusha tff. Kaka usijitoa macho wala usijifanye kiziwi kwa Tff ya Tanzania...kuwa mkweli
    Vipi kuhusu watu walioingia uwanjani toka saa tano waondoke saa tatu uwanjani?
    Vipi usalama wa baadhi ya mashabiki wasiozoeya kuja na kutazama mpira usiku?
    Vipi kuhusu waliokata tiket ya ndege ya saa mbili warudi kwao mwanza kesho wawe kazini? Vipi kuhusu muda wa wachezaji waliofunga kula futari na chakula kumeng'enywa ili wacheze vizuri? Fikilia wanafuturu saa Kumi na mbili na nusu wanacheza saa moja!?? Huu ni mpira? Au ni Pungwa? Hata kanuni za afya haziendi hinyo. Nimegundua mashabiki wengi wa Simba wanajifahamu sana kuliko baadhi ya viongozi wao na hata tff na washirika wake. Tff na washirika wake bmt walijua kabisa kuwa Wakifanya mabadiliko ya ghafla Yanga hawatayaafiki na kwa kufanya hivyo game itahairishwa ili kuifeva timu yao ipate muda wa maandalizi ya mechi zingine...Tff ya karia sio afya katika hii nchi...na waandishi zungumzeni ukweli wa sheria na wala msitafute kupendwa kijinga. Kama mtu anaiba mara ya kwanza na anaachwa, mara ya pili anafanya hivyo hivyo anaachwa mara ya tatu na nne hataiba atanyang'anya na wala hatojua wala kujutia kuwa alikuwa anavunja sheria. Kama kazi ya sheria ni kurinda na kuelekeza wajibu basi vipi Leo tuione busara ni bora? Katika sheria no. 15(10) haijataja neno busara kwahiyo kama unataka busara anza kutumia na kuonesha busara. Prematch meeting hakuna taarifa yeyote, masaa 2 kabla ya mechi unatangaza kusogeza mechi kubwa kama hiyo bila kuwaita wadau wako ukawaambia sababu na usikie mapendekezo yao? SALEHE please acha upapety bro.

    ReplyDelete
  16. Mwandishi anatumia muda mrefu kuhoji Yanga hii inaonekana katumwa kama ni mwandishi Malini Kwa nn asihoji walioahirisha kuwa madhara anayoyaona wao hawakuyaona na Kwa nn kulitolewa muda WA 24 na si masaa sita au mawili ina mana kuna technical reason na ndizo Yanga walikata kucheza wakijua plan ya mpinzani wake ndio mana yeye anaona ni Sawa kuahirisha. Mwandishi yy Hana huruma na mtazamaji aliengia uwanjani asubuhi angoje mechi ya siku usiku kwake yy ni Sawa mtazamaji Hana haki ya Muda ... Tufike mahali tukatae kutumika ili kulinda waluo kidogo ulionayo...

    ReplyDelete
  17. Hapa ni uelewa inawezekena hata naye hajui alichoandika akili ipo Simba tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic