May 31, 2021


 OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa watawakung’uta tena wapinzani wao, Simba watakapokutana katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

 

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, Ruvu Shooting ilishinda bao 1-0 ilikuwa ni zama za Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga na sasa yupo Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 

Amesema kuwa wanajua kwamba wapinzani wao wanafikiria kulipa kisasi ila wasahau suala hilo kwa kuwa halitatokea.

 

“Tunajua kwamba Simba wanafikiria kulipa kisasi, hilo wasahau kwani sisi tupo tayari kuwapapasa, kuwatingisha na kuwakung’uta kwa mara nyingine tena na kujidhihirisha sisi ni zaidi.


"Hakuna namna wachezaji wetu wapo imara na tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu” amesema Bwire.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


Kwenye msimamo, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ina pointi 37 na inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 64.

5 COMMENTS:

  1. Mkwasa yupo kiyanga zaidi kunako mechi ya Simba na Ruvu kuliko kuitafutia Ruvu ushindi. Mechi hiyo Simba itakuwa inacheza na timu tatu yakwanza ni timu ya waamuzi. Timu ya pili ni Yanga na timu yatatu ndio Ruvu yenywe.Timu zotehizi zitakuwa zinapambana kuhakikisha Simba inapoteza mechi hiyo. Tumekuwa tukishuhudia Mara nyingi mechi ya simba na Ruvu huwa ya wachezaji wa Ruvu wanagonga wachezaji wa Simba kwa faulu za kijinga halafu Refa huwa anacheka tu. Mechi hii ya Ruvu na Simba Kuna hatari wachezaji wa Ruvu wakatumika kuwafanyia faulu mbaya wachezaji wa Simba ili kukosa mechi ya Yanga au wachezaji wa Ruvu kutumika kuwatukana baadhi ya wachezaji wa Simba ili kuwaprovok kuchukua maamuzi ya hasira ili kupewa adhabu ya kufungiwa mechi kadhaa ikiwemo mechi ya Yanga. Hii mechi ni mechi itakayojaa uchawi pia. Simba wawe makini na mechi hii ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha uoga wewe Simba wanajua hizo trcks zao zote

      Delete
  2. Simba siyo timu ya kutishiwa nyiau. Bwire ajiheshimu hata ni kazi yake kuongea. Watakula 4-0 ili ajifunze kuwa Simba is on another level.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona mnachachawa nyie mapaka fc msiogope mtapapaswa tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic