May 3, 2021


MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Gwambina FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Badru Mohamed, Meshack Abraham amesema kuwa ofa zote ambazo amepewa kwa sasa ni lazima zisubiri mpaka msimu uishe kwa kuwa wanapambana kubaki ndani ya ligi.

Imekuwa ikielezwa Meshack Abraham anatazamwa kwa ukaribu na Yanga pamoja na KMC ambazo zinahitaji kupata saini ya nyota huyo mwenye uhakika na namba kikosi cha kwanza.

Meshack  mwenye mabao 9 ndani ya ligi akiwa ni amesema kuwa anasubiri kwanza ligi iishe ndipo aweze kuzungumzia kuhusu ofa zake.

“Kwa wakati huu ofa zilizopo ngoja tuzisubirishe kwanza kwa kuwa ligi bado inaendelea na sio wakati wa kuzungumzia hayo hivyo acha kwanza tupambane itakuwa wazi.

“Ni kweli kuna timu ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yangu ila kwa sasa siwezi kuzitaja na sifikirii masuala hayo zaidi ya kuipa mafanikio timu yangu,” amesema.

Gwambina FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ina pointi 30 baada ya kucheza jumla ya mech1 27.

 

 

1 COMMENTS:

  1. Mnyama ingilia kati hapo uvune awe mwenza wa Boko

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic