May 31, 2021


 IMEELEZWA kuwa Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo maarufu kama Carlinhos amevunja mkataba na klabu yake ya Yanga.

Sababu ya nyota huyo kuamua kuvunja mkataba wake huo ni kutokana na matizo ya kifamilia jambo ambalo limefanya aombe kusepa.

Pia nyota huyo alikuwa anasumbuliwa na majeraha jambo ambalo limemfanya ashindwe kuonyesha makeke yake kwenye mechi nyingi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Nelson Mandela wakati ubao uliposoma Tanzania Prisons 0-1 Yanga.

Alikuwa akitibu majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye mchezo huo na hakuweza kumaliza dakika zote 90.

Hivyo amerejea zake nchini Angola kuendelea na masuala yake ya kifamilia pamoja na maisha mengine kuendelea.



6 COMMENTS:

  1. Hapana utulivu hapo

    ReplyDelete
  2. Wasisahau kumsindikiza airport aondoke kama alivyopokewa. Nilisema tangu awali pale hapakuwa na mchezaji

    ReplyDelete
  3. Ameona tangu kufika hapo amekuwa akipambana na nuhusi za kila aina kinyume na matarajio take. Ajiunge na mnyama ikiwa ikiwa Abaco kiwango cha Akina Morrison na Akina Konde boys

    ReplyDelete
  4. Mchezaji hawezi kuwa na kilo 40 akacheza mpira Wale wajinga waliombeba jwa machela sijui wanajisikiaje?

    ReplyDelete
  5. Imeripotiwa kuwa Yanga Sasa wansfanya juu chini aije kujiunga na wekundu WA Msimbazi. Uwovu huo waliokuwa nao ndio chanzo kikubwa cha kutoendelea na lnalosemeksna sio huyo tu lakini wengi wengine wamo mbioni kusepa kuwawacha wananchi mabingwa WA jadi mataani na kuinhia mitini na kugeuga kinyanganyiro baina ya waliokuwa na hela bila ya kutaja majina lakini wajulikana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Andika mambo yanayoeleweka sio kubwabwaja tu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic