KOCHA wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera, kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa suala la yeye kudaiwa kujiunga na Simba kuwa mkuu wa idara ya kusaka vipaji, ataliweka wazi mara baada ya kuingia nchini Tanzania.
Hivi karibuni, kocha huyo alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Gwambina, kabla ya kudaiwa kuachana nao ambapo kwa sasa amekuwa akiendelea na majukumu ya timu ya taifa ya DR Congo kabla ya kuhusishwa kujiunga na Simba akiwa kama Mkuu wa Idara ya Kusaka Vipaji ndani ya timu hiyo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera alianza kwa kucheka kwa muda huku akishindwa kuongea kabla ya kusema kuwa ataweka wazi kila kitu atakapokuwa tayari ameingia nchini.
Zahera hakuweza kukataa wala kukubali juu ya
kujiunga na Simba lakini akasisitiza kuweka
sawa akiwa nchini kwa kuwa bado yupo safarini
kuja nchini kuendelea na michakato yake.
“Nipo Kigali, Rwanda, kuna masuala yangu
nimekuja kuweka sawa, waliniita ila siyo mambo ya mpira lakini nitakuwa nikifika Tanzania nitakueleza.
“Nadhani nikishafika nitakueleza kila kitu juu ya hilo suala lakini kwa sasa hivi sina majibu yake, naomba unielewe ila kwa nini Simba wenyewe wasiwaambie hilo jambo lipoje?” alisema Zahera huku akiendelea kucheka.
0 COMMENTS:
Post a Comment