May 19, 2021


RIPOTI zimeeleza kuwa Klabu ya Chelsea ipo tayari kuweka dau la Euro milioni 80 ili kupata saini ya nyota wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Pamoja na Chelsea kuwa tayari kupata saini ya Sancho, Manchester United na Manchester City ambayo ilikuwa ni timu yake ya zamani msimu wa 2017 nazo pia zinatajwa kuiwinda saini ya winga huyo mwenye miaka 21.

Kocha Mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel anahitaji kufanya kazi na winga huyo raia wa England ili kuongeza makali katika kikosi hicho.

Sancho amekuwa gumzo kwa sasa kutokana na uwezo wake akiwa ametupia jumla ya mabao 16 na pasi 21 katika mechi 37 ambazo amecheza za ushindani wote.

Kiongozi wa masuala ya michezo ndani ya Klabu ya Dortmund, Michael Zorc amesema kuwa wapo kwenye makubaliano na kijana huyo ili kujua hatma yake ndani ya kikosi hicho.

"Tayari tupo kwenye makubaliano na Jadon, tangu mwaka uliopita na kuna makubaliano ambayo tumeyafanya," .



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic