May 11, 2021


TAARIFA kuhusu mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga ambao ulipaswa kuchezwa Mei 8, 202i Uwanja wa Mkapa ila uliahirishwa kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda ule wa awali kwa kuwa ni kinyume na kanuni.

Taarifa iliyotumwa leo Mei 11 kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza kuwa ilipokea maelekezo yaliyotolewa Bungeni  jana Mei 10 na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Usiku wa Mei 10, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amekutana na kufanya kikao na mashauriano na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo Nchini, (BMT) na Klabu za Simba na Yanga.

Taarifa imeeleza kuwa kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Dk. Hassan Abbasi, Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT, Bibi Neema Msita, Rais wa TFF, Wallace Karia na Katibu Wilfred Kidao.

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Bwa.Stephen Mghuto na Mtendaji wake Almas Kasongo. Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na Mjumbe wa Bodi ya Simba, Zacharia Hanspope na kwa upande wa Yanga ni Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla aliyeambatana na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Yanga, Mhandisi Bahati Mwaseba na Kaimu Katibu Mkuu, CPA Haji Mfikirwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa viingilio vitarudhishwa kwa mashabiki 43,947 kwa mashabiki waliokata tiketi zao kupitia N-Card na Waziri amesema amewaomba mashabiki kuwa watulivu katika kipindi hiki na kuiamini Serikali kuwa ilikuwa na nia njema na sababu za msingi iliposhauri awali kwa wadau wa mchezo huo kuwa mechi isogezwe mbele kwa saa chache kabla ya kujitokeza mazingira yaliyosababisha Bodi ya Ligi kulazimika kuaahirisha kabisa mchezo huo.

Kuhusu hatma ya mechi hiyo makubaliano yamefikiwa kuwa mechi hiyo irudiwe ili kuwapa wapenzi wa soka kile walichokitarajia.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:-
 

 



9 COMMENTS:

  1. Hii haina mashiko yoyote, ni maelezo yasiyokidhi kilichotokea na kinachotarajiwa kutokea. Kwanza waziri mwenyewe ndio mshukiwa namba moja wa kuvuruga mambo. Halafu mambo ya yanga kutokuwa na mahusiano mazuri na TFF yanatuhusu nini juu ya mchezo ambao ulivurugwa kwa maksudi na watu wenye malengo duni? Tunataka kujua nani alivuruga mechi sio hizi ngonjera

    ReplyDelete
  2. Wapeni tuu yanga hizo pointi 3 simba haina haja ya kupoteza muda kujiandaa na utopolo tena, watatuumizia wachezaji bure tuu tuna majukumu muhimu kuliko hayo. Labda iwe mechi ya mwisho kabisa na simba wapeleke simba qeens watatosha

    ReplyDelete
  3. Huyo bashungwa tunajua ni yanga, anapanga maamuzi na yanga halafu anayaleta kwenye kikao

    ReplyDelete
  4. Maelezo hayana uzito sema hivi halafu Sema vile ni kitu cha ajabu na kusikitisha sana. Wengi tumeumia na hakuna lililopoza nyoyo

    ReplyDelete
  5. Waziri amaekaa kikao leo na kuamua waliyoamua baadaya kupokea maelekezo toka bungeni na Waziri mkuu..... kwahiyo HUYU Waziri hakuona huo umuhimu mpaka maelekezo yatoke juu kwamba wakae na kuamua..... mbona kama viatu vinampwaya Kabisa ivi

    ReplyDelete
  6. Simba wapeleke U20 au Simba queen watatosha! Wacheza rafu na mpira wa kubutua hawafai

    ReplyDelete
  7. Tatizo ninyi Wala viroba mliogopa Lin up hivyo vichezaji vyenu vinunda vicheze na Wanaume ,mshukuruni KARIA kuwasaidia tungewavunjavunja paka shume

    ReplyDelete
  8. Hapa hata angeingia Barabara akatikisa pasi yake Sarpong aliwapania

    ReplyDelete
  9. We paka kamuulize KARIA, kwanini mechi ilihairishwa kutoka February to may?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic