KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa, amefunguka kuwa amesikitishwa na tukio lililotokea juzi Jumamosi katika mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kuwa wao walijipanga vizuri kwa ajili ya mchezo huo.
Gomes ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kugomea mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa saa 11 jioni kabla ya kubadilishwa muda kwenda saa moja usiku hali iliyosababisha kuzuka kwa tafran.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa hakufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa limewaumiza mashabiki wa soka nchini kwani hakuna aliyetegemea mchezo huo usingekuwepo tena.
“Binafsi naona halikuwa jambo zuri na hakuna ambaye amelifurahia kuanzia kwa mashabiki na wengine katika mchezo wa soka lakini matumaini yetu wahusika watajua nini cha kufanya na kwa wakati gani.
“Lakini nje ya hapo tulikuwa tumejiandaa vizuri kwa mchezo wetu na Yanga, wachezaji walikuwa kwenye morali kubwa ya mchezo lakini maamuzi yaliyotokea ndiyo yamekuwa tatizo kwa kuwa yameumiza wengi,” alisema Gomes.
Watu wasiotumia ubongo wao wamesababisha hili donda kwa wengi. Ni aibu kwa karne hii kukimbia mechi.
ReplyDeleteIkiwa Yanga itaendelea na tabia kama hiyo huko uso I watakuwa wakikimbia sana kila pale wanaohisi mambo si mazuri, lakini wafahamu itabidi mechi zichezwe. Huo ni udhaifu Mkubwa ambapo hapo mwanzo hatujaiona Yanga na tabia kama hiyo
ReplyDeleteWakutoka nduki a.k.a ANZA KANUNI FC
ReplyDeletekanuni wapi wana miaka hata hawafanyi uchaguzi? kanuni kwenye muda..uwajani wapate penalti za nje ya kumi nane...kwao sawa..timu pinzani inyimwe penalti dhahiri shahiri...wao ni sawa..
Deletekanuni isiwe kwenye mpira tu...na katika katiba ya klabu na katikati ya mchezo.pale wangekuwa wacheze na Mwadua na muda ubadilishwe wasingeingia nduki!
ni vema kwa Simba pale Yanga waliamua kutocheza...kwani kwa rafu Yanga ni balaa huenda kuna wachezaji wa muhimu Simba wangeumia katika mechi ile!
simba wangetumia kanuni badala ya busara na viongoz wao wa football failure wangeshinda
ReplyDeleteKanuni zikitumika wanakimbilia kwa Waziri, busara ikitumika wanajificha kwenye kanuni! Hakika tutayaona mengi.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteHiyu waziri ni bomu, muda wowote litaulipua mpira wa Tanzania, sio kwa ushabiki wote huo!
ReplyDelete