May 31, 2021


 BAADA ya mabosi wa Yanga kutangaza kuachana na kiungo wao Carlos Carlinhos imekuwa ikielezwa kuwa huenda akaibukia ndani ya kikosi cha watani zao wa jadi Simba.

Carlinhos raia wa Angola amekuwa akifanya vizuri ndani ya ligi ila amekuwa akisumbuliwa na majeraha jambo mablo limemfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Ana pasi tatu za mabao na amefunga pia idadi hiyo ya mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao sita ambayo ndani ya Yanga kati ya 43 yaliliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili na pointi zake 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Carlinhos hawezi kucheza ndani ya Simba kwa sasa kwani hana uwezo wa kugombania namba katika kikosi hicho.

"Carlinhos kucheza kwenye kikosi cha mabingwa haiwezekani,hilo haliwezi kutokea," amesema.

6 COMMENTS:

  1. Haifa kuwa hata kukaa bench ase duh! Afadhali hata kahata abaki kama mchezaji mbadala wake anakosekana

    ReplyDelete
  2. Ukuma tu huo wa kujitungua habari, hayo kayasema kwenye press conference gani? Acheni ukuma bwana nyie wandishi uchwara

    ReplyDelete
  3. Nani acheze Simba si Bora hata ndemla

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic