THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amewataka wachezaji wake kuweza kuweka rekodi ya kutwaa mataji yote mawili ambayo watacheza fainali katika Kombe la FA pamoja na UEFA Champions League kwa kusisitiza kwamba kazi bado haijfanyika kwa ukamilifu.
Wakali hao wa darajani wana kazi ya kusaka taji la UEFA Champions League mbele ya wababe wa PSG ambao ni Manchester City, Mei 29, Instabul.
Pia Chelsea ina kazi ya kusaka taji la FA mbele ya Leicester City kwenye mchezo wa fainali inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Wembley, Mei 15 jambo ambalo Tuchel ameweka wazi kwamba ni lazima wafanye kazi ya kushinda mataji hayo yote mawili.
Kutinga kwao fainali ya UEFA Champions League ni kupitia kwa mabao ya Timo Werner dakika ya 28 na Mason Mount dakika ya 85 wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid, Uwanja wa Stamford Bridge na kuwafanya watinge hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-1 kwa kuwa nusu fainali ya kwanza ubao ulisoma Real Madrid 1-1 Chelsea.
Lakini Tuchel amesema kuwa kufika fainali pekee haitoshi ni lazima wafanye jambo kwa kutwaa mataji hayo ili wawe kwenye wakati mzuri.
"Tunahitaji kufika katika mwisho mzuri wa fainali ambazo tumefika kwa sasa ili kuwa kwenye wakati mzuri zaidi. Bado kazi haijafanyika kwa ukamilifu. Tunahitaji kwenda katika njia zote ambazo tupo.
"Tunakwenda Instanbul kushinda. Kazi bado haijafanyika kwa ukamilifu. Tukumbuke kwamba tupo kwenye fainali mbili kwa sasa.
"Ninafurahi kwa ajili ya uwezo ambao wachezaji wanaonyesha na tulistahili kushinda kwenye mchezo wetu wa usiku," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment