KUNA hatihati ya nyota wa Yanga, kiungo Carlos Carlinhos kuikosa Simba kwa Mkapa, Mei 8 kwa kuwa bado hajawa fiti kwa ajili ya mapambano.
Ikiwa leo ni Mei 6 bado nyota huyo anasubiri majibu kutoka kwa madaktari ili kujua tatizo lake linalomsumbua ukubwa wake upoje.
Ikumbukwe kwamba Carlinhos mwenye mabao matatu na pasi tatu za mabao alipata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, wakati ubao ukisoma Prison 0-1 Yanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa nyota huyo bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari ambao wanaitazama afya yake kwa ukaribu.
"Madkatari wanaendelea kuangalia kwa ukaribu afya ya Carlinhos kwa ukaribu zaidi na baada ya muda tutatoa taarifa zaidi nini kinaendelea juu yake," .
Ikiwa ataikosa dabi ya Mei 8 nyota huyo atakuwa amekosa dabi zote mbili kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Ile ya Novemba 7 wakati ubao ukisoma Yanga 1-1 Simba zama za Cedric Kaze hakuweza kucheza na hii pia kuna hatihati ya kuikosa tena.
Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa imekusanya jumla ya pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27.
Ikiwa imefunga jumla ya mabao 41 kiungo huyo amehusika kwenye jumla ya mabao sita, akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
Uto imekuwa kama wodi ya wagonjwa sasa kila mtu anaumwa.. inakuwaje mnasajili wagonjwa tu
ReplyDelete