May 13, 2021


 UNAAMBIWA kuahirishwa mechi ya Dabi ya Karikoo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imepora fungu la milioni 200 walizokuwa wameahidiwa wachezaji wa Simba endapo wangeshinda  mchezo huo.


Ikumbukwe kuwa Jumamosi iliyopita, Mei 8, Simba ilitarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, mchezo ambao ulitakiwa kupigwa saa 11:00  kisha kabla ya saa mbili za mchezo kutolewa taarifa na TFF za kusogezwa mbele kisha kuahirishwa kabisa.

Sababu ya mchezo huo kuahirishwa ni kutokana na Yanga kugomea mabadiliko ya muda kwa kuwa ilieleza kuwa yalikuwa ni kinyume na kanuni. 

Kutochezwa kwa mchezo huo kumefanya fuko la milioni 200 ambalo huenda wangepewa kama wangeshindwa kwa kuwa waliahidiwa kuyeyuka jumlajumla.

Chanzo chetu kutoka Simba kimelieleza Spoti Xtra kwamba kama mchezo huo ungepigwa na Simba kuibuka na ushindi, wachezaji wake wangegawana kitita cha milioni 200, walizokuwa wameahidiwa na  uongozi wao.

“Dah! Kuahirishwa kwa mechi Jumamosi kumetunyima hela kabisa, kwani kila mmoja wetu tayari alikuwa ameshajipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili tunapoanza safari ya kwenda Afrika Kusini tuachie familia zetu mpunga huo lakini TFF wametukosesha,” kilisema Chanzo hicho.

Kwa sasa Simba ipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao dhidi ya Kaizer Chiefs ambao ni wa hatua ya robo fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pia TFF imeeleza kuwa mchezo huo utapangiwa tarehe hivi karibuni baada ya pande zote mbili kufikia muafaka.

 

 

 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic