KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ameamua kutumia mbinu za kimafia kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Kaizer Chiefs ambao unatarajiwa kuchezwa Mei 15.
Ikiwa imetinga hatua ya robo fainali ina kazi ya kusaka ushindi katika mchezo wa kwanza wa robo fainai na ule wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 22.
Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa tayari Gomes amempa kazi ya kufanya mtaalamu wao Culvin Mavunga, raia wa Zimbabwe ambaye yeye ni mchambuzi wa mbinu za wapinzani pamoja na mifumo yao.
“Gomes ameshukuru kupewa Kaizer Chiefs, amepanga kuifuatilia kuanzia gemu zao tatu, ajivunia mifumo yao kuwa haina ugumu na amepewa mifumo yao mitatu ambayo wanaitumia.
“Kwa wachezaji wake kawaongezea majukumu ya kufanya na kuwataka wachezaji wake kufuata maelekezo yake, Luis, (Miquissone) amepewa majukumu matatu, kucheza nafasi ya winga, kiungo na beki, Chama, (Clatous) jukumu lake ni umaliziaji,” ilieleza taarifa hiyo.
Kuhusu mchezo huo, Gomes raia wa Ufaransa anayefanya kazi kwa ukaribu na msaidizi wake mzawa, Seleman Matola, alisema:"Hautakuwa mchezo mwepesi kwetu, naamini ushindani utakuwa ni mkubwa ila jambo moja ambalo tunahitaji ni ushindi,".
Ushindi ugenini ni muhimu sana sana
ReplyDeleteSimba naiombea ushindi vs Kaiser chiefs
ReplyDeleteKaizer chief vs simba sc 19:00 usikuuuu jumamosi
ReplyDeleteHongereni sana simba kaiwakilisheni nchi
ReplyDeleteNaitakia Simba yangu ushindi wa bao 3 ugenimi tunamaliza game
ReplyDelete