May 30, 2021

LICHA ya kufikia makubaliano ya baadhi ya mambo kati ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), na klabu ya Yanga katika vikao vyao pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, bado shauri la rufani ya makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela limeonekana kuwa gumu ambapo kwa sasa limepelekwa kwenye kamati ya nidhamu ya bodi ya Ligi.

Aprili 2, mwaka huu Mwakalebela alikutana na rungu la kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano na faini ya Shilingi Milioni 5, baada ya kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuchochea mashabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu.

Akizungumzia suala hilo, Ofisa habari wa kikosi cha klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema: “Sisi tuliipokea ile taarifa ya adhabu ya Makamu Mwenyekiti na kitu cha kwanza ni kuwa tuliipinga kumaanisha ile adhabu hatukukubaliana nayo, lakini pili tulikata rufaa ambayo ilisikilizwa na kamati ya rufani, wao TFF wana mamlaka ya kutangaza nini kimetokea.

“Lakini suala la mwenyekiti na masuala mengine kama tisa ilikuwa miongoni mwa masuala muafaka ambayo Yanga tulikubaliana na TFF, katika vikao vyetu tulivyofanya na Wizara pamoja na TFF, kwahiyo tunaamini TFF watakuwa na majibu mazuri kuhusiana na hilo.

“Sisi kama klabu ya Yanga tumekata rufaa na tunasubiri majibu ya rufaa hiyo, lakini kwa sasa tunaendelea na taratibu nyingine ili kuhakikisha yale yote ya msingi ambayo Yanga wanastahili kuyapata kwa mujibu wa taratibu, Sheria na kanuni na si uonevu yanafanyika.”

Naye Ofisa habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema: “Suala la Makamu mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela kwa sasa lipo chini ya kamati ya nidhamu ya Bodi ya Ligi na kama kutakuwa na majibu yoyote basi mtapewa taarifa.”

5 COMMENTS:

  1. Kwahiyo hiyo kamati ya rufani haijali muda yenyewe hata ikija ipitia hiyo hukumu baada ya mwaka ni sawa tu si ndiyo uonevu wenyewe huo

    ReplyDelete
  2. Hivi hao yanga wao tuu ndio wanataka haki wengine hawastahili haki? Kila siku ni wahuaji wa sheria, taratibu na kanuni wakati wakizivunja na zikatumika kuwaadhibu basi kelele kila siku. Chezeni mpira acheni kutaka mpewe mteremko kisa ni mabingwa wa kulalama

    ReplyDelete
  3. Kuna siku watataka wapewe ubingwa wa mezani

    ReplyDelete
  4. Yaani hata mahakamani ukikata rufaa wewe ndio unapanga muda wa rufaa yako kusikilizwa?Utopolo wamedeka sana.

    ReplyDelete
  5. Mikia imejaa fff

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic