May 30, 2021


UONGOZI wa Azam FC umewapa pongezi nyota wake watano kwa kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kikosi cha Stars kilitangazwa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen Mei 28.

Kinatarajiwa kuingia kambini Juni 5 mwaka huu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Wachezaji wa Azam FC ambao wamejumuishwa kwenye kikosi ni pamoja na Mudhathir Yahya, Salum Abubakar, Bryson Raphael, Ayoub Lyanga na Idd Seleman, 'Nado'.



Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wachezaji hao wanapaswa pongezi kwa kujumuishwa kwenye kikosi hicho na wanapaswa kutimiza majukumu kwa ukamilifu.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic