May 12, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC hautakuwa mwepesi ila wapo tayari kwa ajili ya ushindani ili kupata pointi tatu muhimu. 

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za timu zote mbili ndani ya ligi.

Namungo inapambana kubaki ndani ya ligi huku Yanga hesabu zao ikiwa ni kutimiza jambo lao la kutwaa ubingwa ulio mikononi mwa Simba.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-1 Namungo, ambapo Bigirimana Blaise alikosa penalti baada ya kipa Metacha Mnata kuokoa.

Senzo Mazingiza ambaye ni Mjumbe wa Kamati kuelekea katika mabadiliko ndani ya Yanga amesema kuwa wapinzani wao sio wa kuwabeza.

"Namungo ni timu imara hivyo mchezo wetu hautakuwa rahisi ila kutokana na kikosi tulicho nacho pamoja na mbinu za mwalimu kuna jambo la tofauti linaweza kutokea.

"Kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tupata matokeo kwa kuwa wachezaji wapo tayari kupambana na kupata ushindi,".

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 27 inakutana na Namungo FC iliyo nafasi 11 na pointi 32.

4 COMMENTS:

  1. Hapana haja ya kuzuwa hofu ni timu nyepesi kwani hivi karibu I imekuwa ikifungwa hofu na wala haina staa wa kigeni atayeogopwa

    ReplyDelete
  2. Tumieni kanuni mechi iarishwe.

    ReplyDelete
  3. Watumie kanuni wapewe point 3 za mezani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic