May 12, 2021


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes jana Mei 11 kiliwasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

Mchezo huo ambao ni robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajiwa kuchezwa Mei 15 nchini Afrika Kusini.

Tayari kwa sasa kikosi kimeanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho na  hii hapa ni orodha kamili ya msafara wa wachezaji ambao kwa sasa wapo nchini Afrika Kusini ni pamoja na Aishi Manula, Ally Salim, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Chris Mugalu, Ibrahim Ame.

 Meddie Kagere, Mzamiru Yassin, Fracis Kahata, David Kameta.

Wengine ni Gadiel Michael, Kenedy Juma, Pascal Wawa, Clatous Chama, Taddeo Lwanga, Larry Bwalya, Hassan Dilunga, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu, Joash Onyango, John Bocco na Luis Miquissone.

3 COMMENTS:

  1. Hapa lilipita kosa kuhusu upatikanaji wa viza ya Morrison kwani tatizo hilo bila ya shaka likijulikana tangu mwanzo na ilibidi lishughulikiwe mapema, lakini kinachoharibika hutengezeka na iwe fundisho

    ReplyDelete
  2. Hapo hatoki mtu. Ni timu mbili kamili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic