NYOTA wa AS Vita, Djuma Shaban amesema kuwa akijiunga na Klabu ya Yanga baada ya uataratibu wa dili lake kukamilika atahitaji kuvaa jezi namba 21.
Beki huyo raia wa Congo inaelezwa kuwa amemalizana na mabosi wa Yanga kwa dili la miaka miwili ambapo amesema kuwa akija anahitaji kuvaa jezi namba 21.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa dili lake na AS Vita linameguka Juni 30 hivyo ikiwa atakuja Bongo basi atafanya kazi na mabosi wake wapya kwa ajili ya kuyatafuta mafanikio.
Kwa upande wa wachezaji wa Simba ameweka wazi kwamba hakuna ambaye anamvutia kwa sasa licha ya kikosi hicho kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yeye kajiunga yanga, fine, kuna haja gani ya kuzungumzia wachezaji wa simba? Nilitegemea aseme wachezqji wa yanga wanaomvutia sio simba.
ReplyDeleteKabla hujalaumu fikiria kwanza chanzo cha habari kimetoka wapi
DeleteHilo ni garasa tu na muda ukifika itadhihirika. Atajua SIMBA si timu ya mchezo mchezo
DeleteSawa mkuu nimekuelewa
ReplyDelete