June 11, 2021

 


GADIEL Michael nyota wa kikosi cha Simba inaelezwa kuwa jina lake limewekwa kando kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.


Nyota huyo ambaye ni beki wa kushoto aliibuka ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes akitokea Klabu ya Yanga.


Habari zinaeleza kuwa kushindwa kufiti kikosi cha kwanza ni sababu inayofanya nyota huyo kupigiwa hesabu za kuachwa.


Uwepo wa beki ambaye ni nahodha, Mohamed Hussein, 'Tshabalala' kuwa katika ubora ni sababu inayofanya uongozi wa Simba kufikiria kumuacha.


Kuhusu suala la usajili, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah, 'Try Again' amesema kuwa muda wa usajili bado na mipango yote ipo kwa kocha.

2 COMMENTS:

  1. Hiyo ndiyo faida ya ulimbukeni mi nadhani Simba wabaki naye tu huku kwetu Yanga ,Ajibu sijui Gadiel Michael Ni virusi hawana nafasi Tena hata wasisogee kabsa.

    ReplyDelete
  2. Gadiel ni simba damu, bora ajibu,

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic