KIUNGO wa Azam FC, Salum Aboubakary, 'Sure Boy' anatajwa kuwa katika rada za mabosi wa Yanga huku wenye mali nao wakihitaji huduma yake.
Ikumbukwe kuwa msimu uliopita wa 2019/20, Yanga walikuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo ambapo ishu ilikuwa katika dau.
Yanga wao waliweka dau la milioni 40 jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Azam FC wawaambie kwamba waongeze dau kwa kuwa Sure Boy ni nembo ya Azam FC jambo lililokwamisha dili hilo.
Kwa sasa mkataba wa nyota huyo ambaye yupo katika kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars unakaribia kumeguka jambo ambalo linawapa nguvu Yanga kuipata saini yake.
Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria alisema kuwa ni ngumu kwa timu hapa Bongo kumchukua mchezaji ambaye anahitajika na Azam FC.
"Kwetu sisi Azam FC kumuacha mchezaji tunayemtaka labda tuamue sisi ila hakuna ambaye anaweza kushindana nasi, kama biashara sisi tunafanya mpaka tuamue wenyewe," .
Pes za yanga ni kutokana na ruzuku za kugsiwa sio kwa jasho lak sio kama Simba na Azam
ReplyDeleteWalimtaka Sure Boy ati kwa 40 milioni waliona nyingi za kuishtuwa Azam. Hahahaaa
ReplyDeleteNdio thamani sahihi, nyinyi mnaopigwa na mawakala endeleeni
ReplyDeleteHatutaki wazee hacha kufunga story,sure boy kachoka nashangaa hata Stars kaitwa kwa lipi.
ReplyDelete