KOCHA mkuu wa kikosi cha
klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa wamejipanga kucheza kama fainali
mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, ili kutangaza ubingwa wao wa
nne mfululizo wa Ligi Kuu Bara.
Simba inayoongoza msimamo
wa ligi na pointi zao 73 baada ya kucheza michezo 29, wanahitaji pointi tatu
pekee kutangaza ubingwa wao wa nne mfululizo, huku wakijipanga kuwakaribisha
Yanga katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa
Mkapa Dar es Salaam Julai 3, mwaka huu.
Katika mchezo wa mzunguko
wa kwanza wababe hao walipokutana, matokeo yalikuwa sare ya bao 1-1, mchezo
uliopigwa Novemba 7, mwaka jana.
Akizungumza na Gomes amesema: “Tunafurahia kwa muendelezo wa ushindi tulionao, hii
inazidi kutupa hali ya kujiamini kuelekea mchezo wetu ujayo dhidi ya Yanga.
“Tunatarajia kucheza
mchezo huo kama fainali, ili kutangaza ubingwa wetu wa nne mfululizo, tuna
michezo mitano mbele yetu na tunahitaji ushindi mmoja pekee, naiamini timu
yangu na natumaini tutafanya vizuri mpaka mwisho wa msimu.
“Kuhusu Chama huyu ni
mchezaji wetu muhimu, anakuwa na mchango mkubwa kikosini, tulipanga kumpa
dakika 30 kwa ajili ya kuanza kumuandaa kuelekea michezo yetu ijayo, hasa ule
wa nusu fainali dhidi ya Azam na pia mchezo dhidi ya Yanga.”
Sawa
ReplyDeleteKiuhalisia Yanga haipo vizuri kwa Simba. Kuna kelele nyingi zinapigwa kuwa mechi ya Watani haitabiriki ila kutokutabirika huko kwa sasa kunategemea zaidi imani za kishirikina na Yanga kuelekea kwenye mechi hii wameekeza zaidi kunako masuala ya kishirikina kupata matokeo kuliko kiwango na uwezo wao wa mpira uwanjani. Ukiwaangalia simba wapo consistency yaani kiwango Chao hakijashuka labda kuongezeka kwa muda Sasa. Wapewe tu ubingwa watuongezee timu kimataifa.
DeleteHii jeuri ya Gomes inatokana na sisi wenyewr Yanga. Sisi kwa sasa ni ukweli usopingika kiwango chetu ni kibovu sana. Wachezaji hawana mbinu. Wachovu. Kocha wetu anajaribu kuziba viraka lakini kama wavoona wazee ni afadhali kuacha kutia tumu maana wao wamekusudia ktuuwa
ReplyDeleteKumbe kutangaza ubingwa kitu ambacho ni yakini mnaita jeuri. Kosa lenu Nyinyi ni mpaka mechi kabla ya Mbeya City bado mkiamini ubinngwa utakuwa wenu na mpaka leo hii wapo wasiokuwa na akili eti Simba watafungwa mechi zijazo na nyinyi ndio mabingwa. Tarehe tatu hiiko mbali
ReplyDeleteUbingwa wa yanga ni kuifunga Simba hakuna ubingwa mwingine wanaotaka yanga wao hawitaji kombe wakiifunga Simba basi tayari wanajiona mabingwa ndio maana wanasema ubingwa bado hauna mwenyewe
ReplyDeleteHahaha Utopolo bana ati ubingwa hauna mwenyewe!! Hamko serious kabisaa
ReplyDeleteMbona kuna kipindi simba ilikua iteremke daraja lkn ili mfunga Yanga, kwahiyo derby sio nyepesi kama baadhi ya mashabiki wapya mnavyofikiria, mchezo wa mpira sio hesabu za kutoka kichwani inategemea sana Game plan ya siku husika usiishi kwa kukariri...
ReplyDeleteKILA KILICHOPITA HAKIWEZI KUBADIRIKA, YAJAYO YANATEGEMEA UWEZO WETU
Delete