June 20, 2021


RAZACK Siwa, Kocha wa Makipa wa Yanga amesema kuwa wanaweza kumtumia kipa namba tatu, Ramadhan Kabwili katika mechi zilizobaki ikiwa ni pamoja na ya leo dhidi ya Mwadui FC, Uwanja wa Mkapa.


Ikiwa mzawa Kabwili ataanza leo kukaa katika mlingoti wa lango la Yanga utakuwa mchezo wake wa kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ambapo Yanga imecheza jumla ya mechi 30  yeye hakuanza hata mchezo mmoja.

Pia Kabwili atakuwa ni mbadala wa kipa namba moja Metacha Mnata ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na suala la utovu wa nidhamu.

Alizungumza na Saleh Jembe, Siwa amesema kuwa kuna mechi ambazo zimebaki wanaamini wataweza kumtumia Kabwili ambaye hajapata nafasi ya kucheza.

Siwa amesema:-"Nafikiri mechi bado hazijaisha hivyo tumuombe Mungu nafikiri kwa mechi ambazo zimebakia tunaweza kumuona Ramadhan Kabwili akianza kwani huwa ninafundisha kila mchezaji kuweza kupata nafasi ya kucheza.

"Ninarudia kusema kuwa mapumziko tuliyopata wakati ule wa timu ya taifa yametufanya tuwe imara hivyo tunahitaji kupata matokeo chanya katika mchezo wetu dhidi ya Mwadui FC," amesema Siwa.

Nahodha Msaidizi Ramadhan Kabwili amesema kuwa anaamini kuwa mechi sio kazi ngumu kuliko mazoezi hivyo yupo tayari kucheza. 

"Ninaamini kwamba mazoezi ni magumu kuliko mechi hivyo kwangu mimi nipo tayari tusubiri tuone kocha atampanga nani kama ataanza Shikalo, (Farouk), kama ni Metacha, (Mnata) sawa sisi wote ni timu moja tunahitaji ushindi,"  amesema Kabwili.

Frederick Masombola, Kocha Msaidizi wa Mwadui FC, amesema kuwa kupoteza mechi mbili mbele na Yanga kumewaongezea umakini hivyo watapambana kupata ushindi.

"Tumecheza mechi mbili na Yanga ile ya mabao 5-0,(ligi) na ule wa pili tulifungwa mabao 2-0,( FA) hivyo tumejipanga na wachezaji wapo tayari kisaikolojia ukizingatia kwamba wapo wengine ambao tuliwasajili dirisha dogo hawakuwepo mechi ya kwanza," amesema.

Mussa Mbissa nahodha wa Mwadui FC amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kutafuta ushindi Kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.


5 COMMENTS:

  1. Hiyo mussa mbisa ndiye aliyempora mpira beki wake kisha akampa mchezaji wa yanga afunge bao au mwingine? Mwadui waandike maumivu na leo.

    ReplyDelete
  2. Nakumbuka bara a la ugundi lilikwisha kutamka kuwa Kabwili yupo njiani kutemwa lakini leo inafikiria yeye ndie ataemaliza mechi zilizobakia. I Jee akipata msumivu nani atakuqa mbadala na jee tunataraji nini ikiwa ameshajuwa Kuwa atatemwa kwakuwa Hana kiwango?

    ReplyDelete
  3. Kocha aachiwe huru kufanya maamuzi. Naomba tusimuinhilie. Leo mwadui hatoki

    ReplyDelete
  4. Kua watu bila kutaja Yanga kwa ubaya wanaweza kufa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic