June 20, 2021


KLABU ya Arsenal  inayonolewa na Kocha Mkuu, Mikel Arteta ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya Andre Silva ili awe mbadala wa Alexandre Lacazette.

Mshambuliaji huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Eintracht Frankfurt anatajwa kuwa chaguo la kwanza la Arteta ambaye anahitaji kusajili kwenye eneo la ushambuliaji.

Mpango wa Arteta ni kumuuza Lacazette na kumsajili Silva ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ndani ya Ligi Kuu England pamoja na mashindano mengine.

Lacazette msimu uliopita alibeba Arsenal ambayo ilimaliza nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi na ndiye mfungaji bora wa kikosi hicho akiwa ametupia mabao 13.

Silva ndani ya Bundesliga alikuwa na msimu bora kwa 2020/21 alitupia jumla ya mabao 28 na pasi 10 akiwa nafasi ya pili kwa ufungaji nyuma ya kinara wa utupiaji ambaye ni Robert Lewandowski aliyetupia mabao 41 na dau lake linatajwa kuwa ni pauni milioni 34.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic