June 11, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kinaendelea na program zake kama kawaida kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu aliliambia Spoti Xtra kuwa wachezaji wanaendelea na program kama kawaida licha ya ligi kusimama kutokana na uwepo wa kambi ya timu ya taifa ya Tanzania inayojinoa kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Kikosi hicho kilianza program yake Juni 8 baada ya mapumziko waliyopewa kukamilika na jana pia waliendelea na mazoezi Viwanja vya Simba Mo Arena huku Gomes akitarajiwa kurudi kutoka nchini Ufaransa Juni 11ambayo ni leo.  

Mchezo wao ujao kwenye ligi ni Juni 19 ambapo itakuwa ni dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa CCM Kirumba. 

Mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-0 Polisi Tanzania.

"Kila kitu kipo sawa na tayari wachezaji wanaendelea na mazoezi ambapo wakati mwingine wanakuwa uwanjani na muda mwingine gym," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic