June 1, 2021


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa nyota wao Carlos Carlinhos aliomba kuondoka yeye mwenyewe jambo ambalo liliwafanya wamruhusu pia wameongeza kuwa hakuwa akifanya program aliyopewa na madaktari.

Jana Mei 31, Carlinhos alivunja mkataba na mabosi wake Yanga kwa makubaliano ya pade zote mbili baada ya kuzungumza.

Anasepa Yanga akiwa amecheza kwenye jumla ya mechi 15 katika mashindano yote ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa:"Ni kweli suala hilo limetokea ili klabu isiwe na mzigo na yeye awe na furaha kama ambavyo aliandika kwenye barua yake.

"Wakati timu ikiwa Shinyanga unajua yeye aliumia akiwa Ruangwa, madaktari walimuwekea programu ya kufanya ila hakuwa akifanya hivyo," .

Nyota huyo ameshareja nchini kwake Angola akiwa amenyanyua taji moja ambalo ni Kombe la Mapinduzi na hakucheza hata mchezo mmoja Visiwani Zanzibar kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha.


3 COMMENTS:

  1. Hii sio muhimu, mwacheni aondoke. Labda kama mnataka kufanyia mizengwe kama morrisson

    ReplyDelete
    Replies
    1. Morrison sio mizengwe, lipeni chetu yaishe

      Delete
  2. Nani atamchukua mgonjwa huyo nyie

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic