SASA ni rasmi klabu ya Yanga imemsainisha beki wa kulia wa AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo Shabani Djuma kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
Djuma Shabani unakuwa ni usajili wa kwanza wa Yanga wa kimataifa ambapo klabu hiyo imelenga kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo timu hiyo inanafasi kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Yanga chini ya Mwenyekiti msaidizi wa kamati ya usajili Eng. Hersi Said amesema kuwa timu hiyo itafanya usajili wa maana kwa ajili ya kufanya vizuri kwa msimu ujao katika mashindano yote ambayo watashiriki.
Akizungumzia usajili wa beki huyo Meneja mkuu wa AS Vita, Yves Dida Ilunga alikiri wazi kuwa klabu ya Yanga tayari imekamilisha usajili wa beki huyo na hivi karibuni watatangaza dili hilo.
“Kila kitu kimekamilika, Yanga imeshakamilisha taratibu zote za kumsajili Djuma, nadhani hivi karibuni kila kitu kitakuwa wazi juu ya dili la beki huyu, tunasubiri taratibu tu za timu ila kila kitu kimemalizika,”
Kwa upande wa meneja wa mchezaji huyo Faustino Mukandila yeye amesema kuwa “Yanga imefanikiwa kumsajili mteja wangu Shabani Djuma, hivyo watu wafahamu kuwa kila kitu kimekamilika siku sio nyingi tutangaza dili hilo kuwa lipo tayari,”
Naye Nahodha wa klabu ya AS Vita na timu ya taifa ya Congo, Jeremy Mumbere alifunguka juu ya dili la nahodha mwenzake wa klabu hiyo Shaban Djuma juu ya kujiunga na Yanga ambapo amesema: "Tayari Shabani Djuma amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga, mimi tayari ameniaga kuwa atajiunga na Yanga mara baada ya kumalizika kwa mchezo wetu wa mwisho wa ligi tutakaocheza Juni 6 mwaka huu.
“Ameniambia kuwa amesaini mkataba na Yanga wa miaka miwili, hivyo baada ya mchezo wa mwisho ataanza mipango ya safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.”
Naye Shabani Djuma mwenyewe tulipomtafuta kuzungumza kuhusu usajili wake wa kujiunga na Yanga amesema kuwa “Nafikiri taratibu zilizobaki ni kwa upande wa klabu ya Yanga na AS Vita kuweka wazi dili hilo, nachofahamu kila kitu kimekamilika nasubiri wao waweke wazi ishu hii ili kila mtu afahamu kinachoendelea,”
Alipotafutwa Makamu mwenyekiti
kamati ya Usajili ndani ya Yanga Eng. Hersi Said kuzungumzia juu ya usajili wa
beki huyo simu zake ziliita bila majibu.
Anakaribishwa
ReplyDeleteKwani wao wenyewe wanasemaje?au wanabisha?
ReplyDeleteWanasubiria mkampokee kama Calinhyo
Delete