UONGOZI wa kikosi cha klabu ya KMC umefunguka kuwa kulipa kisasi kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Dodoma Jiji.
KMC na Dodoma jiji zitakutana Juni 17, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mara ya mwisho kwa KMC na Dodoma Jiji kukutana ni katika mchezo wa hatua ya 16 bora ambapo Dodoma walishinda mabao 2-0 na kutinga robo fainali ya michuano hiyo ambapo waliondoshwa na Simba kwa mabao 3-0.
Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa habari wa klabu ya KMC, Christina Mwagala amesema: “Kikosi chetu kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma jiji, ambapo makocha wanaendelea na programu zinazofanyika kwenye viwanja vya hoteli ya White Sand.
“Kwetu mchezo huu ni wa kisasi
baada ya Dodoma Jiji kutufunga katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya
kombe la Shirikisho msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment