June 1, 2021

 



HABARI kutoka ndani ya kikosi cha klabu ya AS Vita zinaeleza kuwa beki wa kulia wa timu hiyo, Shaban Djuma hivi karibuni aligoma kusaini mkataba mpya kwa ajili ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Shabani Djuma mwenye uraia wa DRC Congo, ambaye ndani ya AS Vita  ni nahodha wa klabu hiyo, amekuwa anahusishwa kutakiwa na klabu ya Yanga, ambao mpaka sasa wapo kwenye mazungumzo.

Akizungumzia mustakabali wa dili hilo, Meneja wa mchezaji huyo, Faustino Mukandila amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo amegoma kusaini mkataba mpya kwa kuwa anataka kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, huku akithibitisha kuwa kwenye mazungumzo na Yanga.

“Ni kweli Djuma alipewa mkataba mpya na uongozi wa AS Vita lakini amegoma kusaini mkataba huo, yeye  ameniambia kuwa anahitaji kupata changamoto mpya baada ya kuitumikia AS Vita kwa muda mrefu.

“Kwa sasa tupo katika mazungumzo na Yanga lakini hayajakamilika, Yanga wameonyesha nia ya kweli na tayari wameshaleta ofa yao ambayo bado tunaijadili, kama mambo yatakwenda vizuri huenda akajiunga na Yanga.

Shabani Djuma licha ya kuwa beki wa kulia wa timu hiyo lakini amefanikiwa kufunga mabao 6 na kutoa pasi 5 za mabao katika ligi kuu ya nchini DRC Congo maarufu kama ‘Linafoot’.


8 COMMENTS:

  1. Huyo atakeenda kupokelewa Marsidis is a na mstarumbeta ya miezi that is Micha he watamuona hafai and na hata Kuan a kumzomea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona aliwakimbiza sana mpaka ulimi nje

      Delete
    2. Ala kikatokea nini baada ya kukimbia kwake hovyo!?

      Delete
  2. YANGA NI MIONGONI MWA CLUB ZINAZOTUMIA MUDA MWINGI NA NGUVU NYINGI SANA KUSHAWISHI MASHABIKI ZAO WAAMIN KITU AMA JAMBO AMBALO KIUHALISIA HALIPO,NA DHAMIRA KUU YAKUFANYA HIVI NI KWAMBA UKWELI WANAUFAHAMU KATIKA MAMBO MATATU 1;YANGA NI KLABU ILIYOSHUKA KIWANGO CHAKE KWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI NA KUTHIBITISHA HILO HUU NI MSIMU WA NNE AU TANO SIMBA WANAENDELEA KUBEBA UBINGWA LIGI KUU,2;WAMEJITAMBUA KWAMBA HATA WAFANYE NINI HAWAWEZI KAMWE KUA SAWA NA SIMBA HIVYO WANATUMIA MBINU MBADALA KUWAHADAA MASHABIKI,MFANO MATUMIZI YA MEDIA KAMA GAZETI,REDIO BLOGS SOCIAL NETS NA TV,3;KESI YA BM3 HAIPO CAS TAS UKITAKA KUAMIN INGIA WEBSITE YA CAS THEN TAFUTA DATABASE SITE AMBAYO INAONYESHA KESI ZOTE ZA MIAKA YOTE NA KAMWE HUTAONA KESI YA BM3 NA JIULIZE KWANINI SIMBA INAPOELEKEA KUTAWAZWA KUA BINGWA NDIO MNAANZA KELELE,KWANINI TANGU MWANZO MLIKUA MMENYAMAZA?HII NI ISHARA KWAMBA YANGA MASHABIKI WAKE HAWAJIELEWI NA WANADANGANYWA SANA,MNGEHOJI KUHUSU MUANGOLA NA SIO BM3 ACHENI KUPOTEZEWA MUDA NA KUZUGWA AKILI.,4;USAJILI WA WACHEZAJI AMBAO TAYARI NI MAGARASA MFANO SAIDO,FISTON,SAPPONG,CALINHO,YIKPE NA WENGINE WENGI SANA.KWAKUHITIMISHA YANGA ITAKUJA KUPATA ANGUKO LAKUDUMU MUDA SIO MREFU NA MKIFANYA MCHEZO HATA NAFASI YA PILI MNAWEZA MSIIPATE MKACHEZO SHIRIKISHO NA SIO KLABU BINGWA AFRIKA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo timu ikifanya vizuri hufichwamabaya yake lukosa na chikwende sio mizigo simba wamepigwa hamsemi yanga ikikosa ubingwa haiwi ya nne bado itakuwa nafasi za juu ubingwa yanga hakosi kiwanjani anakosa nje timu gani inangoza kukataliwa magoli halali na pernati halali tathimini kama mwanamichezo simba wanawazidi yanga nje ya uwanja sio ndani na mwisho unakuja

      Delete
    2. Hauko seriuos yaani ule mpira wanaoupiga Simba unalinganisha na utopolo wenu halafu unasema yanga wanazidiwa nje ya uwanja na sio ndani. Angalia hata ubora wa wachezaji wa simba halafu na utopolo wako ni tofauti kabisa. Kwahiyo utasema pia hata uwezo wa simba kimataifa ni TFF au ni mipango nje ya uwanja?

      Delete
  3. Kwani kisinda amewafanyia nn yanga tangu amefika?zaidi yakukimbia kimbia tu la maana hakuna,endeleeni kukusanya wanariadha kwasababu mnataka kushiriki mashindano ya riadha,umemuona kagere ana mbio bocco ana mbio?ila ndio top score vpl na ataendelea kusumbua.

    ReplyDelete
  4. SIMBA ISINGEKUWA NI TFF UBINGWA WASINGECHUKUWA. ANAYEJUA MPIRA UKWELI ANAUJUA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic