July 18, 2021


 KLABU ya Al Ahly ya Misri imefanikiwa kutetea taji lake la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ubao wa Uwanja wa Mohammed V kusoma Kaizer Chief 0-3 Al Ahly kwenye mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

Kipindi cha kwanza ngoma ilikuwa nzito kwa timu hizo zote ambazo ziliwahi kucheza na Klabu ya Simba ya Tanzania kwa nyakati tofauti ambapo Al Ahly mabingwa walicheza na Simba katika hatua ya makundi na Kaizer Chiefs ilicheza na Simba katika hatua ya robo fainali.


Ni mabao ya Mohamed Sherif dk 53, Mohamed Magdy Afsha dk 64 na Amr El Solia dk 74 yalitosha kuwapa taji hilo waarabu hao wa Misri.


Nyota wa Kaizer Chiefs, Happy Mashiane hakuweza kumaliza fainali hiyo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu dk 45+4 na kuwafanya wacheze wakiwa pungufu washkaji zake.


Jumla mashuti ambayo Al Ahly ilipiga yalikuwa ni 17 na mashuti manne yalilenga lango huku Kaizer Chiefs ikipiga mashuti matatu na ni moja ambalo lililenga lango.

13 COMMENTS:

  1. Hii ndio ushahidi mkubwa kuliko yote ya nguvu na ubora za Simba ambapo Al Ahli iliyotwaa ubingwa katika msimu huu haikufungwa na timu yoyote isipokuwa na Simba tu na pale Simba ilipokwenda Misri ilifungwa kwa bao moja tu na tena kwa tabu Na hapo ndipo Simba iliyetoa fursa kwa timu nyengine kujiunga na mashindano hayo msimu ujao lakini kuna wanaoyachukia haya na kuendelea kubeza kama walivokuwa siku zote yaani mafanikio na furaha za Za Simba kwa wengine misiba mikybwa sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaizar chiefs kiherehere tu. Kwenda kuicheza ngoma isiomuhusu akashindwa kuendana na mdundo.Simba watanzania ndio tuliosababisha kushindwa kufikia malengo. Simba walikuwa wanapambana na hujuma za pande tano kwa wakati mmoja.(1) kaizer chiefs wenyewe.(2) Uongozi wa chama Cha mpira wa Africa kusini akiwemo Raisi wa CAF ambae ni msauzi(3) Alhaly na Masomane wake ambao hawakutaka hata kidogo kukutana na Simba kwenye hatua inayofuata.(5)Yanga na Senzo.Hawa ndio wapishi wakubwa wa matokeo walioyapata kaizer chiefs kwa Simba home and away. Watanzania tunaroho mbaya kweli na sio hadithi za midomoni hatupendi mwenzetu afanikiwe hata kama na sisi wenyewe tunanufaika ndani yake na mafanikio ya mwenzetu.Hapa nakumbuka hadithi ya Mtanzaniia alieomba Dua ili apate kile alichokuwa anakitaka hasa utajiri na Mungu alimkubalia kwa sharti kuwa chochote kile atakachokiomba lazima jirani yake apate mara mbili zaidi ya yeye lakini Cha kushangaza Mtanzaniia yule aliomba upofu wa macho ili jirani yake asione macho yote mawili yeye abakiwe na jicho moja huyu ndie Mtanzaniia halisi ndani ya roho yake. Hatariii.

      Delete
  2. Imeshawaumiza na kuanza kulalama kwa uchungu na wataumia

    ReplyDelete
  3. Wa bongo kwa story za kuunga tupo vzr kwavile Simba alimfunga Al-Ahly,
    Simba ni bora kuliko Ahly,
    Kwahiyo Yanga alimfunga Simba ndio tuseme Yanga ni bora kuliko Simba na Ahly?
    Nafikiri tujipange kinachotakiwa kubeba kombe sio kuungaunga story tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna aliposema Simba ni bora kuliko ahly, hauko makini Kama timu yako ilivyo

      Delete
  4. paformence ya timu pamoja umakini na nizamu wa timu
    ndi vigenzo

    ReplyDelete
  5. hatungalii nani kamfunga nani lazima uliemfunga awe anashiriki mashindano ya kimataifa hapa ishu ya simba na yanga haina nafasi muache yanga ajitahidi alete heshina kama anavyo fanya simba infizwe kwenye vigezo vya ubora kimataifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ingekuwa unajibu swali la kwenye mtihani invigilator angekuwekea bonge la mkasi na kuchora kibonzo cha mtu zuzu!!

      Delete
  6. Simba bana.Haaaaa Ubingwa wa Africa sio maneno.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila wa ligi kuu bara ndo maneno

      Delete
  7. Ila wa ligi kuu bara ndo maneno

    ReplyDelete
  8. Hadithi uliyoizungumza yaweza kufananishwa na roho mbaya za Yanga, yeyote machafu ya nchi hii unayoyaona, mwanzilishi Yanga. Hii ni ukweli kabisha, wakubali au wakatae lakini ndio uhalisia kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic