July 7, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya KMC, umefunguka kuwa, timu yao ipo kwenye maandalizi mazuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Simba hawaendi kukamilisha ratiba ya kuwapa ubingwa wapinzani wao hao.

 

KMC leo Julai 3 watakuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Simba ikiibuka na ushindi kwenye mchezo huo, itakuwa bingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha pointi 76 ambazo Yanga inayoshika nafasi ya pili inaweza kuzifikia ikishinda mechi zake mbili zilizosalia, lakini itazidiwa uwiano wa mabao na kuifanya Simba kuwa bingwa kabla ya kumalizia mechi tatu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala, alisema: “Tunaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa Jumatano, ni wazi tunatarajia mchezo mgumu kwa kuwa wapinzani wetu ni timu bora, na wanatoka kupoteza mchezo muhimu wa dabi.

 

“Hivyo malengo yao makubwa yatakuwa kusaka ushindi kwa namna yoyote ile, ili wajipoze na ubingwa, lakini niwaweke wazi kuwa tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi ya kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huu, na hatuwezi kukubali kutoa tiketi ya ubingwa bali tutapambana kufanikisha malengo yetu.”


Kwenye msimamo, KMC ipo nafasi ya 6 ina pointi 42 baada ya kucheza mechi 31 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza imecheza mechi 30 ina pointi 73. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic