July 4, 2021

 


KIUNGO Charles Zulu ni suala la muda tu kwa sasa kutambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Azam FC baada ya kukamilisha masuala ya vipimo leo Julai 4.

Kiungo huyo ambaye ni raia wa Zambia anaibuka ndani ya kikosi cha matajiri wa Tanzania, akitokea Afrika Kusini, abapo alikuwa anacheza ndani ya Klabu ya Cape Town City.

Taarifa rasmi iliyotolewa leo na Azam FC imeeleza kuwa kiungo huyo tayari amekamilisha utaratibu katika vipimo hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni suala la makubaliano ya nyota huyo kusaini dili la kuwatumikia mabosi hao wanaoutumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi zao za nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic