KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum ‘FeiToto’, amefunguka kuwa baada ya kukamilisha michezo yao ya Ligi Kuu Bara, sasa wanajipanga vizuri na mchezo wa fainali ya shirikisho dhidi Simba utakaopigwa Julai 25, mkoani Kigoma huku akiahidi kuwa kuna Sapraizi wamewaandalia Wanayanga.
Vigogo hao wa soka la Tanzania watakutana kwenye mchezo wa fainali hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Yanga wataingia katika mchezo huu na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, kwenye mchezo wao wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Julai 3, mwaka huu.
Fei Toto amekuwa kwenye fomu ya hali ya juu, chini ya kocha Nasreddine Nabi, ambapo mpaka sasa msimu huu nyota huyo amefanikiwa kufunga mabao matano.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Fei Toto alisema: “Kiukweli kila mchezaji ndani ya kikosi chetu ana ari kubwa kuelekea mchezo wetu wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, bila shaka utakuwa mchezo mgumu kwa sababu ni fainali na kila timu ina malengo ya kushinda kombe hilo.
“Lakini niwaahidi Wanayanga kuwa kuna kitu cha tofauti wanakwenda kukipata kwenye mchezo huo, hivyo wasikose kujitokeza kutusapoti kwa wingi," .
Sawa mzee
ReplyDeleteKelele nyingiiiii
ReplyDeleteShida huyu anamtaja Fei hili ,mi.mpanie au achungwe ,lkn mjue bila mechi za kupanga Chama mechi ya Yanga na Louis Ni ngumu kwao ,vile vioski viliondoka amebaki Lamine naye tumemlisha Yamin kujifanya kaumia nk
ReplyDeleteKajifunze kwanza kuandika ndo uje humu
DeleteHata sijaelewa alichoandika
ReplyDeleteHatari na nusu umeandika Kitu gn we jamaaa htukuelewi ujue una fanya mpaka Pilau nililo kula nili tapike
ReplyDelete