July 20, 2021


 WACHEZAJI wa zamani waliocheza kwa mafanikio ndani ya Yanga, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani wamefunguka kuwa wao kwa sasa hawana mpango wa kuagwa na klabu yao hiyo kwa kuwa bado wanaendelea kucheza soka.

 

Ngassa na Yondani wametoa kauli hiyo baada ya wadau mbalimbali kuzua mjadala wa kwa nini Yanga hawajafanya sherehe za kuwaaga wachezaji hao ambao wamecheza kwa muda mrefu zaidi ndani ya kikosi hicho kuliko Niyonzima ambaye aliagwa juma lililopita.

 

Meneja wa Ngassa ambaye yupo karibu na Yondani, Godlisten Anderson (Chicharito), aliliambia Championi Jumatatu kuwa wachezaji hao wamekataa kuagwa na Yanga kwa sasa kwa sababu bado wanaendelea kucheza soka na wanaamini mchezaji anayeagwa ni yule ambaye anastaafu.

 

“Kiukweli mimi binafsi nimewashauri Ngassa na Yondani wakubali kuagwa na Yanga kama mwenzao Haruna kama viongozi wakitaka kufanya hivyo lakini wote wamekataa kabisa ishu hiyo kwa sasa.

 

“Hoja yao wanasema kuwa bado wapo kwenye gemu sana na wachezaji wanaoagwa ni wale ambao wanaachana na masuala ya soka. Hivyo wao wanaona hadi siku wakistaafu ndipo wafanyiwe sherehe ya kuagwa,” alisema Chicharito.

 

Ngassa anamalizia maisha mafupi ya mkataba wake ndani ya Gwambina ambao unafikia ukomo baada ya ligi kumalizika, wakati Yondani yeye anatumika ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania.

5 COMMENTS:

  1. Wewe Mwandishi yule Captain wa Netherland ex Liverpool mbona aliagwa na yupo PSG.Hapa Ni Elimu wewe na wao inawamaliza

    ReplyDelete
  2. Kwa ufupi Yondani na Ngasa ni wachezaji wenye ari zao na kutojifanya cheap walwaondosha walipoona hawawataki

    ReplyDelete
  3. Kujifanya Cheap kwani Polisi alipo Yondani Kuna maisha gani,la Mudamu mfano eti wasaidiwe ,acheni story zisizo na kichwa na miguu kwani kuagwa Hatuna imekukwaza Nini? Unafunga story unajibu wewe ,Kama Mchezaji Ana hatred hatuwezi kumbadili kakataa Yanga Mishahara anataka Signing fee Sasa huko Polisi anapata Nini? Ajali tu wanaongea eti baord ya Ligi iweke BIMA wao walioanzisha Timu hawakujua risks Kama wapo expensive then wasitulilie Lakini jua Hatuna kaagwa end of story

    ReplyDelete
  4. Ìmenishangaza, hivi Ngassa na Yondani wanapokataa kuagwa wanamkomoa nani; Yanga, Gwambina au Polisi?
    Na je, nani aliwaomba awaage?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic