July 23, 2021


 KAMA mpango wa Yanga wa kuachana na wachezaji wake, Lamine Moro na Michael Sarpong ukatimia, basi huenda mshambuliaji wa AS Vita, Fiston Mayele na beki wa DC Motema Pembe, Henock Inonga wakachukua mikoba yao.

 

Lamine na Sarpong, inaelezwa kwamba mwishoni mwa msimu huu watapewa mkono wa kwaheri ndani ya kikosi hicho huku sababu kubwa ikiwa ni utovu wa nidhamu.

 

Chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, kamati ya nidhamu ya timu itakaa kuwajadili. Na tayari ilishawajadili ambapo Lamine alionekana kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Dodoma Jiji huku Sarpong akikosekana.


Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, mbali na hilo, hivi sasa Yanga ipo katika mazungumzo ya kuwasajili wachezaji wawili, mshambuliaji na beki mmoja wa kati ambao ni Henock Inonga na Fiston Mayele.

 

"Kamati ya Nidhamu ya Yanga hivi karibuni itakaa kujadili mambo mengi yaliyojiri ya kinidhamu, hivyo suala la Lamine Moro na Michael Sarpong yatajadiliwa, kisha kurudishwa kamati tendaji na hapo ndiyo itafahamika kama wachezaji hao watabaki Yanga au wataondoka.

 

“Lakini hayo yakiendelea, Yanga pia ipo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao ni mshambuliaji wa kati na beki mmoja wa kati kwa ajili ya kukiimarisha kikosi kuelekea msimu ujao.

 

"Wachezaji hao ni Henock Inonga anayecheza nafasi ya beki wa kati na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji wa kati, hayo ni moja kati ya majina yaliyomo katika orodha ya wachezaji walio katika mazungumzo na uongozi wa Yanga,” Kilisema chanzo hicho.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominick Albinus, aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Kila kitu kuhusu maamuzi ya wachezaji wenye matatizo ya kinidhamu yanafanyiwa kazi na Kamati ya Nidhamu ya Yanga," .

3 COMMENTS:

  1. Mnasajili timu 2 tofauti au?

    ReplyDelete
  2. Taarifa zako zina jirudia rudia tu hazina mashiko unataka kupoteza fans kuwa makini sisi ni wasomaji wakubwa wa makala sasa hii iko hovyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic