MSHAMBULIAJI wa DR Congo, Fiston Mayele, amesema kuwa ana uhakika wa kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha Yanga katika msimu ujao wa mashindano yote itakayoshiriki klabu hiyo.
Mayele ambaye alikuwa ni mshambuliaji wa AS Vita, anatajwa kutua Yanga na tayari mwenyewe amethibitisha kutua hapa nchini hivi karibuni.
Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele alisema amekifuatilia kwa karibu kikosi cha Yanga na kisha kusema kuwa anaiona nafasi yake ya kucheza msimu ujao huku akikisifia kiwango cha mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne.
“Yanga nimekuwa nikiifuatilia tangu nifahamu kuwa wananihitaji, wana kikosi kizuri ila nimeona kuwa katika eneo la ushambuliaji bado kuna tatizo hivyo naiona kabisa nafasi yangu ya kucheza nikiwa kama mshambuliaji pale.
“Nimemuona mshambuliaji Yacouba Songne katika michezo yao ya mwisho ambayo nimeitizama, ni mchezaji mzuri lakini pia Mukoko Tonombe na Tuisila Kisinda ni wachezaji wazuri, naamini ni msaada mzuri kwa timu,” alisema mshambuliaji huyo.
Fiston Mayele ndiye alikuwa mshambuliaji tegemeo wa Klabu ya AS Vita ambapo msimu huu katika michezo ya ligi kuu, amefanikiwa kuifungia timu yake mabao 13 huku akiwa mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo.
Mayele amesema ameona kwenye nafasi ya ushambuliaji kuna tatizo hivyo amekuja yeye.... Karibu mkombozi wetu
ReplyDeleteYaap
DeleteTunatunza maneno yako ndugu mayele ila usije ukaomba kuondoka kabla ya mkataba kuisha
ReplyDeleteAmtafute Fiston Abdulrazak au Yikpe wampe habari
DeleteMajembe fc
ReplyDeleteIla timu ya Yanga kwa kuchagua majembe kwa kweli ni wazuri sana.
ReplyDeleteHahahaa, majembe kama wakina namanyele
DeleteMajembe kama Barbara
ReplyDelete