TIMU ya taifa ya Italia imetinga hatua ya fainali ya Euro 2020 baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Hispania kwenye mchezo wa nusu fainali.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa Uwanja wa Wembeley ambapo Italia walianza kupachika bao la kuongoza dk ya 60 kupitia kwa Federico Chiesa.
Mshambuiaji wa Hispania, Alvaro Morata aliweka usawa bao hilo la awali la Italia dk ya 80 na kufanya dk 90 za awali ubao kusoma Italia 1-1 Hispania.
Sasa Italia wametinga rasmi kwenye hatua ya fainali ambapo wanaweza kucheza na England ama Denmark Uwanja wa Wembley itakuwa ni siku ya Jumapili ambapo bingwa wa Euro 2020 atajulikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment