July 7, 2021


 SHABIKI na Mwanachama maarufu wa Klabu ya Yanga mzee Haji Mpili ameweka wazi kuwa ushindi wa bao 1-0, walioupata dhidi ya Simba, Julai 3, 2021 yeye ndio alicheza mchezo huo na kuhakikisha Simba haishindi.

 

Mzee Mpili ambaye alionekana na baadhi ya viongozi wa juu wa Yanga siku kadhaa kabla ya mechi amesema alichokifanya kwa Mkapa ni siri yake na atakifanya tena kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Azam Federatio kati ya Yanga na Simba, itakayochezwa katika Uwaja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 25, 2021.

 

“Hii ya tarehe 3 ilikuwa salamu tu derby yenyewe ni tarehe 25 Kigoma kwa sababu Simba wana kelele sana na kelele zao tunajua akina nani wanawapa hizo kelele, mimi ndo nilikuwa mchezaji namba moja wa ule mpira na Kigoma ndo utachezwa mpira wa uhakika.

 

“Mchezo wa Kigoma nimeshamaliza kazi, Kigoma hawatoki ng’ooo, niache kama nilivyo hawatoki. Wapeni habari kwamba Mzee Mpili amesema kama alivyowafungeni Dar es Salaam na Kigoma mtafungwa, tena magoli ya Kigoma ni ya kuhesabu.

 

"Nilijua tutashinda, hata kama Simba angetangulia kufunga ningesawazisha na kuongeza goli la pili. Tunajua Simba inajipanga kulipa kisasi kwenye mchezo wa Fainali ya FA lakini tayari wamechelewa Kigoma wanakufa tena na shughuli imeisha, tunawapiga tena.

 

“Nimepewa guarantee asilimia 100 kuwa mechi ya Kigoma imeisha na tutashinda goli mbili kwenda mbele. Kama wanasema Jumamosi tulibahatisha sawa. Lakini Shughuli yote wataiona kigoma, hatuwezi kuliacha hilo Kombe,” amesema Mzee Mpili ambaye kwa sasa ana-trendi mitandaoni kila kukicha.

 

Yanga inasubiri kukutana na Simba kwa mara ya nne kabla ya kukamilisha msimu huu huku ikiweka rekodi ya kutokufungwa na Simba kwenye michezo mitatu mfululizo.


Kwenye ligi ilikuwa mechi mbili ambapo ile ya awali ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba, ule wa pili ulisoma Simba 0-1 Yanga na wa awali ilikuwa ni Kombe la Mapinduzi, Zanzibar, Yanga ilishinda kwa penalti 4-3.

5 COMMENTS:

  1. Ngoma ikivuma mno haikawii kupasuka, aendelee kurapu tuu

    ReplyDelete
  2. Kila masika na mbu wake...Zimeisha enzi za Pierre Liquid sasa zimekuja enzi za Mzee Mpili

    ReplyDelete
  3. Huyu mzee aambiwe kuwa soka cku hz n la science halisi,, uchawi hauna nafasi tena. Na kwa maendeleo ya soka la tanzania, vitendo vya kishirikina vipingwe vikali sana la cvyo hatutakuwa na timu bongo. Wachezaji hawatofanya mazoezi badala yake wataenda kwa kina mpili na wenzie! Poor mzee mpili

    ReplyDelete
  4. Well said hata siku ya mechi ya simba na kaizer chief kuna shabiki alikua anavunja nazi ,na kwenye mechi ya simba na as vital club mashabik waliingia na paka huo ni ushirikina wa wazi kabsa haitakiwi kufumbia macho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic