BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga, Dickson Job amesema kuwa hawakuwa na msimu mzuri ndani ya 202021 kwa kuwa hawajapata taji la ligi.
Beki huyo zao la Mtibwa Sugar ameweka wazi kuwa jitihada zao hazikuweza kufanikiwa hivyo wataongeza zaidi kwa msimu ujao wa 2021/22.
Ikumbukwe kwamba Job ni ingizo jipya kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na alikuwa ni chaguo lake la kwanza katika mechi za kumalizia msimu.
Ni mafasi ya pili Yanga imemaliza kwa msimu wa 2020/21 kwenye mashindano ya ndani ambapo katika ligi ni namba mbili na pointi 74 na kwenye Kombe la Shirikisho ni ya pili huku namba moja akiwa ni mtani wake Simba.
Job amesema:"Hatukuwa na msimu mzuri kwa kuwa tulihitaji kutwaa taji kwa ajili ya Wananchi ila haikuwa hivyo. Kwa mapokezi yao makubwa na sapoti yao tunashukuru,"
Kwani lile la mapinduzi sio taji
ReplyDeleteAhsanteni kwa kushiriki. Karibuni tena msimu ujao
ReplyDeleteKombe la mapinduzi halitambuliki na CAF. Tunaweza kusema ni kombe la ndondo ama la kahawa
ReplyDeleteYale ni mashindano ya ndani. Ndo maana mchezaji yoyote hata asiposajiliwa anaweza kushiriki
ReplyDelete