July 29, 2021

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba, Meddie Kagere amewasilisha kwa uongozi wa Simba barua ya maombi ya kutaka kusitisha mkataba wake ndani ya klabu hiyo kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, huku ikielezwa kuwa muda wowote huenda akajiunga na Yanga ambayo imekuwa ikimnyemelea.

Kagere amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Simba msimu huu, kutokana na ushindani mkubwa wa namba kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo hasa kutokana na usajili wa Straika, Chris Mugalu.

Kwa muda wa misimu mitatu ambayo Kagere ameichezea Simba kwenye Ligi Kuu Bara pekee Kagere amefanikiwa kuifungia Simba mabao 58, kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara pekee, ambapo msimu wa 2018/19 alifunga mabao 23, 2019/20 mabao 22 na msimu wa 2020/21 mabao 13.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba kimefunguka kuwa, Kagere alikutana na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji juzi Jumanne usiku, ili kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

“Ni kweli Kagere amekutana na bosi MO, kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kufikia makubaliano ya pande zote mbili na kuachana na Simba, hii ni kutokana na mchezaji huyo kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya klabu ya Simba.” kimesema chanzo hicho.

Alipotafutwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu kuzungumzia suala hilo amesema: “Kwangu binafsi nisingependa kuliongelea suala ambalo bado halijafanyiwa uamuzi na bodi ya Wakurugenzi, subiri mpaka tutakapokaa na kufikia uamuzi na tutatoa taarifa.”

Shangwe limehamia Kwa upande wa Yanga ambapo moja Kati ya viongozi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema: "Msimu huu lazima tutawashangaza watu kwa kusajili mchezaji mkubwa kutoka katika moja ya Klabu kubwa Tanzania, jambo ambalo linaashiria huenda akawa ni Meddie Kagere," amesema kiongozi huyo.

 

 

8 COMMENTS:

  1. Weka kipengere kama cha kalinyos, hakuna kusajiliwa timu yoyote ndani ya ligi kuu mpaka miaka 4 ipite

    ReplyDelete
  2. Aya bana tunamtakia maisha mema

    ReplyDelete
  3. Si jambo kubwa kwani kwa muda wa misimu mine iliyopita Simmba ilizowa wachezaji kadhaa wa Yanga ambao wapo mpaka leo wamecheza kwa mafanikio makubwa na huyu Kagere pia na wengineo walikuwa ndani ya rada za Yanga lakini Simba akawatoa tonge kinywani waachiwe nao wamchukue kwani Simba wameshafaidika nae bao akiwa fresh

    ReplyDelete
  4. Mwacheni aende akakuze kiwango halafu tutamrudisha kwenye timu kubwa

    ReplyDelete
  5. SIFA KUBWA YA SIMBA NA MM NI MWANACHAMA NI KUACHA WACHEZEJI WAZURI KWA FITINA ZAO ZA KISHENZI NA KUCHUKUWA WACHEZAJI WABOVU UKWELI NDIO HUO

    ReplyDelete
  6. Simba tunafanya fault kubwa kumuacha Kagere,sababu iliyosabibisha cyo kwamba ameshuka kiwango ni fitina za viongozi na Matola.Ukweli utabaki kuwa ukweli,Kagere ni bora kuliko Bocco na Mugalu hilo halipingiki,misimu 2 mfungaji bora,msimu mmoja pamoja na kucheza match chache magoli 13,lazima tukubali ukweli Wana Simba tuache kuwa na fitina kwa wachezaji wenye viwango vikubwa,hayo ndiyo yanayomkuta Chikwende ,hachezeshwi halafu wanatudanganya kwamba haendani na mfumo was coach,kweli mpira wa Bongo kichefuchefu.Wakina Mess na Christian Ronaldo cyo waspaniola lakini hawafanyiwi figisu za kipuuzi,bora Luis Miqssuine aondoke zake la cyvo yatamkuta ya Kagere

    ReplyDelete
  7. Yanarudi ya tambwe ngoja mtajionea wenyewe huyu mwamba akitua jangwani hali itakua ngumu sana kwa simba kuchukua ligi kuu.yanga haina striker anayejua lango

    ReplyDelete
  8. Wakimtaka yanga watoe pesa bado anamkataba .porojo za yanga .munamtaka kaeni mezani utapolo fc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic