July 29, 2021

BAADA ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, Kiungo mshambuliaji wa Yanga Feisali Salum ‘Fei Toto’ amefunguka na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kutokata tamaa kwani wanaenda kujipanga ili kufanya vizuri msimu ujao.

Katika  msimu huu wa Ligi Kuu Bara alifanikiwa kuifungia timu yake ya Yanga   mabao matano na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumzia mipango yao, Feitoto amesema kuwa mashabiki wa timu yao wasikate tama kwani mambo mazuri yanakuja msimu ujao wanaendelea kujipanaga kurejesha furaha ya mashabiki wao.

“Tunawaomba mashabiki  wetu  wasikate tama  kwani mambo mazuri yanakuja waendelee kuwa pamoja na sisi, na tunawashukuru sana kwa sapoti wanayotuonyesha na tunawaahidi kufanya vizuri msimu ujao.

“Msimu huu hatujafanikiwa kufikia malengo yetu lakini hatuja kata tama tunaendelea kujipanaga ili kuhakikisha tunafanya vizuri zaidi na kutimiza malengo yetu,”amesema Feisal.

3 COMMENTS:

  1. Msimu ujao, msimu ujao, msimu ujao, ... Ni upi huo mbona haufiki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi Simba bado ni wepesi Fei Toto?

      Delete
    2. Nadhan sasa hivi anajutia kauli yake maana nafsi inamsuta

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic